MAGAZETI ya Leo Ijumaa 18 July 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 18 July 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 18 July 2025

Serikali imetangaza kuwa moja ya shabaha kuu katika Dira 2050 ni kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia pato la Taifa lenye thamani ya Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, pamoja na kuongeza wastani wa pato la mtu mmoja kufikia Dola 7,000.
Akizungumza katika uzinduzi wa dira hiyo Alhamisi ya Julai 17, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema:
“Mheshimiwa Rais, Dira ina shabaha 18, na ya kwanza na kubwa kabisa ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na pato la Taifa lenye thamani ya Dola za Marekani trilioni moja na wastani wa pato la mtu mmoja wa Dola 7,000,”
Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, kufikia lengo hilo kutahitaji ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi, uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu, na utekelezaji wa sera madhubuti za uchumi na maendeleo.
