NAFASI Za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili

NAFASI Za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili
NAFASI Za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026 Awamu ya Pili
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) anatangaza nafasi za Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi.
Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 02) pamoja na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati.
Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali Msingi na Elimu Maalumu (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).
Waombaji wa nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).
Mafunzo haya yatatolewa katika
Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali.
Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) ni:
- Wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
- Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali au Msingi.
- Aidha waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa, watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa
wa Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu.
Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) ni
wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer
Studies au Computer Science.
AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya Mafunzo ya Ualimu (kozi) na vyuo vinavyotoa mafunzo husika.
A.STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI (MIAKA 02)

B.STASHAHADA MAALUMU YA UALIMU ELIMU YA MSINGI KATIKA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI (MIAKA 03)
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NA KUPOKEA MAJIBU.
Utaratibu wa kutuma maombi na kupokea majibu utakuwa kama ifuatavyo:
- Wahitimu wa Kidato cha nne, Kidato cha sita na Walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobainishwa katika tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi.
- Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://tcm.moe.go.tz/).
- Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
- Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
- Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia “Account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 18/08/2025) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
- Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo visivyo vya Serikali watatuma maombi yao katika vyuo husika.
- Aidha, majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo hayo yatatolewa na Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa na.
- Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake.
- Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 14/08/2025.
Tags: NAFASI Za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2025/2026
