Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

Filed in Michezo by on 19.09.2025 0 Comments
Share This Post
Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuujulisha umma kuwa, imekubaliana na waendeshaji wa timu ya Tabora United kuimiliki timu hiyo ambayo sasa itajulikana kwa jina la TRA United Sports Club.

Timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu ya mpira wa Miguu ya Tanzania (NBC Premier League) ni ya Walipakodi na Watanzania wote.

Hivyo, kwa sasa itabaki katika Mkoa wa Tabora.

TRA United Sports Club pamoja na kuwa ni timu ya mpira wa miguu ambayo itatoa burudani kwa walipakodi na Watanzania kwa ujumla, pia itakuwa na malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo:-

Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

Tabora United Sasa ni TRA United Sports Club

  • Kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari.
  • Kutoa elimu ya masuala ya kodi na umuhimu wa kulipa kodi.
  • Kueneza ujumbe wa uzalendo na uwajibikaji wa kodi kwa maendeleo ya Taifa.
  • Kuendeleza vipaji vya michezo nchini.
  • Kuimarisha uwajibikaji wa kijamii kupitia michezo kwa kuongeza ajira kwa watanzania katika sekta ya mpira wa miguu kama inavyofanyika na timu za Mpira wa Miguu za Mamlaka za Mapato katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (Corporate Social Responsibility).

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaomba ushirikiano wa wadau wote kwa timu hii ambayo ni ya walipakodi na watanzania wote, ili kutimiza azma ya Taifa letu ya kujenga uchumi imara kupitia ulipaji wa kodi wa hiari.

“TRA United – “Kodi Yetu, Maendeleo Yetu.”

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *