MAGAZETI ya Leo Alhamisi 02 October 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 02 October 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 02 October 2025

Mahakama ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemuhukumu adhabu ya kifo aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, bila ya yeye kuwepo Mahakamani.
Hukumu hiyo imetolewa Jumanne na Mahakama ya Kijeshi ya DRC kutokana na mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya Kabila kwenye mahakama hiyo Julai 25, 2025.
Kiongozi wa jopo la majaji sita waliosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Kijeshi, Luteni Jenerali Joseph Mutombo Katalayi, amesema Kabila alikutwa na hatia ya makosa mbalimbali yakiwemo uhaini, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji, unyanyasaji wa kingono, mateso na uasi.
“Kwa kutumia Kifungu cha 7 cha Kanuni ya Adhabu ya Kijeshi, Mahakama imeamua kutoa adhabu moja tu, ambayo ni kali zaidi, nayo ni adhabu ya kifo,” alisema Luteni Jenerali Katalayi wakati akisoma hukumu hiyo.
Pia, Kabila alituhumiwa kushirikiana na kikundi cha waasi cha M23 linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, ambalo liliteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa Congo mwanzoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo, Rwanda ilikanusha kutoa msaada wa kijeshi kwa M23, lakini wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanasema jeshi la Rwanda lilikuwa na mchango mkubwa katika mashambulizi ya kundi hilo.
