NAFASI 35 Za Kazi Manyoni District Council

NAFASI 35 Za Kazi Manyoni District Council
NAFASI 35 Za Kazi Manyoni District Council
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. HW/X.1/1 VOL.III/176
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni anapenda kuwatangazia Wananchi wote wenye Sifa kujaza nafasi 35 Za kazi zifuatazo hapa chini.
✅WATOZA USHURU KATIKA VYANZO MBALIMBALI VYA MAPATO (NAFASI 30)
SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) na kuendelea Mwenye uzoefu na kazi ya kutoza ushuru na matumizi ya POS na mwenye rekodi ya uadilifu atapewa kipaumbele.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTOZA USHURU
- Kuhakikisha kila anayepaswa kulipia ushuru na tozo za Halmashauri katika chanzo cha kukusanya/kizuizi analipa ushuru stahiki.
- Kuhakikisha kuwa fedha zote zilizokusanywa zinawekwa benki sio zaidi ya masaa 24 kutoka zilipokusanywa.
- Kuhakikisha POS wakati wote zipo salama na zinafanya kazi bila kuwa na matatizo.
- Kuripoti tatizo lolote la POS kwa Wataalam wa IT kwaajili ya marekebisho.
- Wakati wote kuwadhibiti wakwepa ushuru hata ikibidi kuripoti ngazi ya Halmashauri kwa hatua zaidi.
- Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri/ Msimamizi wako.
✅ASKARI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI (NAFASI 05)
SIFA ZA KUAJIRIWA
- Awe amehitimu Darasa la Saba na Kuendelea ambaye anaweza kusoma na kuandika vizuri na awe amehudhuria na kufaulu mafunzo ya Mgambo yanayotolewa na jeshi letu la Wananchi na kutunukiwa cheti cha kuhitimu.
KAZI NA MAJUKUMU YA ASKARI
- Kushiriki operesheni mbalimbali za usafi wa mazingira, malipo ya tozo mbalimbali za Halmashauri.
- Kuhakikisha usalama kwenye maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu.
- Kuhakikisha wananchi wanatekeleza sheria mbalimbali za Serikali kuu na Sheria ndogo za Halmashauri.
- Kudhibiti watoroshaji wa bidhaa mbalimbali zinazopaswa kulipiwa ushuru wa Halmashauri.
- Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na Mwajiri/ Msimamizi wako
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na Mkazi wa Manyoni.
- Awe na umri usiozidi miaka 45 Waombaji wawasilishe maelezo binafsi (Wasifu) yenye Anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
- Waombaji waambatishe nakala za vyeti Kidato cha Nne (Form IV) na Kidato cha Sita (Form VI), Taaluma na Cheti cha Kuzaliwa.
- Waombaji watakaowasilisha “Result Slip”,”Statement of Result”, “Provisional Results”, au “Tanscripts” HAVITAKUBALIKA.
Barua za maombi zilizosainiwa na mwombaji zinaweza kuandikiwa kwa lugha kiingereza na Kiswahili.
Maombi yatayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili HAYATAFANYIWA KAZI.
Maombi yatumwe kupitia anuani ya:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni,
S.L.P 60,
MANYONI.
ENZI MTENDAJI (W)
YAMANYONI
Mwisho wa Kuwasilisha Maombi ni tarehe 20/07/2025.
