WALIOITWA Kwenye Usaili Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa (MUCE) July 2025

Filed in Ajira by on 15.07.2025 0 Comments
Share This Post
WALIOITWA Kwenye Usaili Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa (MUCE) July 2025

WALIOITWA Kwenye Usaili Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa (MUCE) July 2025

WALIOITWA Kwenye Usaili Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa (MUCE) July 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26 hadi 27 Julai 2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
    Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
    Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
    vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyet vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha kubadili Jina (Deed poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *