NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kwa Kozi za Muda mrefu Katika Vyuo Vya VETA 2026

Filed in Elimu by on 18.07.2025 1 Comment
Share This Post
NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kwa Kozi za Muda mrefu Katika Vyuo Vya VETA 2026

NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kwa Kozi za Muda mrefu Katika Vyuo Vya VETA 2026

NAFASI Za Kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi Kwa Kozi za Muda mrefu Katika Vyuo Vya VETA 2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inakaribisha maombi ya kujiunga na Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Ngazi ya Kwanza kwa mwaka wa mafunzo utakaonza Januari 2026 kwenye Vyuo vinavyomilikiwa na VETA.

SIFA ZA KUJIUNGA
Mwombaji anatakiwa awe;

  • Mtanzania mwenye umri kuanzia Miaka 13 na Kuendelea.
  • Na Cheti cha kuhitimu Elimu ya Msingi na/ au Kidato cha nne na kuendelea.

UTARATIBU WA KUOMBA

  • Maombi yatafanyika kupitia mfumo (online application) wa VETMIS, unaopatikana kwenye tovuti ya VETA (www.veta.go.tz) au kwa nakala ngumu (hard copy) za fomu zinazopatikana kwenye vyuo au tovuti ya VETA.
  • Malipo ya Fomu ni Shilingi 5,000 (Elfu Tano tu) na yatalipwa kwa Namba ya Malipo (Control Number) ambayo itatolewa wakati wa kurejesha fomu chuoni au kuwasilisha kwenye mfumo.
  • Muombaji anatakiwa kurudisha fomu iliyojazwa akiambatisha nakala ya cheti cha kuzaliwa, vyeti vya Elimu aliyonayo pamoja na picha ndogo tatu (3) zenye usuli (background) wa rangi ya buluu.
  • Fomu zitarejeshwa kwenye Chuo husika au kwa njia mtandao (Online) kupitia Mfumo wa VETMIS kwenye Tovuti ya VETA (www.veta.go.tz).

KIPINDI CHA MAOMBI
Fomu zitatolewa kuanzia tarehe 19 Julai 2025 na mwisho wa kuchukua na kurudisha Fomu ni tarehe 30 Septemba 2025.

ADA KWA MAFUNZO YA NGAZI YA KWANZA

  • Ada ya kutwa: 60,000/=
  • Ada ya bweni:120,000/=
  • Gharama nyingine zimeainishwa kwenye fomu ya kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa chuo husika.

Ufundi Stadi Fursa kama zote kwa Watu Wote Karibu ujiunge na Elimu na Stadi kwenye Vyuo vya VETA.

Kwa Maelezo na Ufafanuzi zaidi, wasiliana nasi:
VETA Makao Makuu,
12 Barabara ya VETA, 41104 Tambukareli,
S. L. P. 802, Dodoma
Barua pepe: info@veta.go.tz au pr@veta.go.tz Simu: +255 26 2963661
Simu ya mkononi: 0755 26 74 89
ya Ufundi

Share This Post

Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Haleluya loti kyomo says:

    Napenda kusoma vyuo vya ufundi sitadi tz kama utaona pendekezo language niite

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *