NAFASI 17 Za Kazi Mtibwa Sugar Estates Limited

NAFASI 17 Za Kazi Mtibwa Sugar Estates Limited
NAFASI 17 Za Kazi Mtibwa Sugar Estates Limited
Mtibwa Sugar Estates Limited ni kampuni inayojishughulisha na uzalishaji wa miwa na utengenezaji wa sukari katika eneo la Mtibwa – Turiani – Mvomero – Morogoro Tanzania.
Sifa mojawapo ya Mtibwa Sugar ni kufanya kazi kwa ushirikiano (teamwork).
Mtu yeyote anayefanikiwa kuwa miongoni mwa wafanyakazi wa Mtibwa Sugar anakuwa mwanafamilia wa Mtibwa Sugar na hatajuta kwa maamuzi yake hayo kwani atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wenzake na Utawala kwa ujumla.
Pia Mtibwa Sugar inajali kukuza vipaji na fani mbalimbali kwa wafanyakazi wote.
Nafasi 17 Za Kazi zilizotangazwa na Mtibwa Sugar Estates Limited ni kama ifuatavyo;
✅Mwanasheria (Legal Officer) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe Wakili.
- Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 5.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45
✅Mkaguzi wa ndani (Internal Auditor) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na shahada ya uhasibu.
- CPA ni lazima.
- Uzoefu wa kazi za ukaguzi wa ndani usiopungua miaka 5.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45
✅Afisa Mazingira, Afya na Usalama mahala pa kazi (EHS Officer) nafasi 5
SIFA ZA MWOMBAJI
- Shahada ya kwanza ya Uhandisi, mazingira, afya, usalama mahala
pa kazi au inayoendana. - Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45.
✅Msimamizi wa Ubora (Quality Supervisor) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Shahada ya usalama wa chakula au inayoendana nayo.
- Uzoefu wa kazi usiopungua miaka 3.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45.
✅Meneja wa Ubora, Usalama, Afya na Mazingira (SHEQ Manager) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Shahada ya kwanza ya Uhandisi, mazingira, afya, usalama mahala pa kazi au inayoendana.
- Uzoefu usiopungua miaka 4 (minne) katika ngazi ya Meneja katika eneo husika.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45
✅Afisa Tabibu (Clinical Officer) nafasi 2
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amesajiliwa na awe na leseni hai inayomruhusu kufanya kazi ya Afisa tabibu.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka 2.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45.
✅Daktari (Medical Doctor) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe amesajiliwa.
- Awe na leseni hai.
- Uzoefu kazini usiopungua miaka 2.
- Awe Mtanzania.
- Umri usiozidi miaka 45.
✅Afisa kumbukumbu Mwandamizi (Senior Records Officer) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na Shahada katika fani ya kumbukumbu.
- Awe na uzoefu katika usimamizi wa kumbukumbu kama Mkuu wa Kitengo kwa muda usiopungua miaka 5.
- Awe na umri usiozidi miaka 45.
- Awe Mtanzania.
✅Mtawala wa Hospitali (Hospital administrator) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na Shahada ya Usimamizi wa mifumo ya Afya.
- Awe na uzoefu wa kazi katika usimamizi wa Hospitali usiopungua
miaka 5. - Awe na umri usiozidi miaka 45.
- Awe Mtanzania
✅Mtaalamu wa matengenezo ya vifaa au mashine kiwandani kulingana na hali halisi ya vifaa au mashine Maintenance Technician (CBM) nafasi 1
SIFA ZA MWOMBAJI
- Stashahada katika Uhandisi wa Mitambo au umeme.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka 2 katika viwanda vikubwa.
- Awe na umri usiozidi miaka 45.
- Awe Mtanzaniag
✅Mwanafunzi mhitimu katika uhandisi wa vipimo (Graduate Trainee in Instrumentation Engineering) nafasi 2
SIFA ZA MWOMBAJI
- Shahada ya uhandisi wa umeme na elektroniki.
- Awe na umri usiozidi miaka 35.
- Awe Mtanzania
Maombi yote yatumwe kwa barua pepe Hr@mtibwa-sugar.co.tz au yapelekwe katika ofisi za HR – MTIBWA au yatumwe kwa njia ya POSTA.
Meneja Rasilimali Watu na Utawala, S.L.P 42, Mtibwa, Morogoro.
Mwombaji aambatanishe wasifu (CV), picha yake ya hivi karibuni (passport size), leseni ya fani husika, vyeti, TIN, NIDA au kitambulisho cha kura na cheti cha kuzaliwa.
Angalizo
- Mwombaji awe tayari kufanya kazi na kuishi Mtibwa.
- Mwombaji asiwe na rekodi ya kukutwa na hatia ya jinai mahakamani
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 31/07/2025.
