TETESI Za Usajili Ligi Kuu ya Tanzania 2025/2026

TETESI Za Usajili Ligi Kuu ya Tanzania 2025/2026
TETESI Za Usajili Ligi Kuu ya Tanzania 2025/2026
✅Klabu ya Mtibwa Sugar ipo kwenye mazungumzo na Beki, Vicent Andrew “Dante” ambaye ni Mchezaji huru baada ya mkataba wake na KMC Fc kumalizika.
✅Paul Peter amejiunga na JKT Tz akiwa Mchezaji huru Kutoka Dodoma Jiji FC.
✅Klabu ya Namungo FC imekamilisha usajili wa Beki, Abdallah Mfuko Kutoka Kagera Sugar FC.
✅Vilabu vya Mashujaa na Namungo vimeshatuma ofa ya kuhitaji huduma ya Fadhili Mwinyimvua Kutoka Dodoma Jiji FC.
✅Vilabu vya KMC, Mbeya City, na Mtibwa Sugar vipo kwenye vita Kali ya kuwania saini ya kiungo wa kati Geoffrey Manyasi.
✅Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Enoch Lihonzasia Kwa mkataba wa miaka 2 Kutoka AC Rangers ya nchini Congo.
✅Pacome ZouZoua na Max Nzengeli wameongeza mkataba wa miaka 2 kuendelea kuitumikia Young Africans.
✅Nassoro Kapama amejiunga na Tabora United Kama Mchezaji huru Kutoka Kagera Sugar FC.
✅ LKlabu ya Dodoma Jiji FC imekamilisha Usajili wa golikipa, Castor Mhagama Kutoka Ken Gold FC.
✅Klabu ya Namungo FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Heritier Ebenezer Makambo Kutoka Tabora United FC.
✅Klabu ya Mashujaa FC imekamilisha Usajili wa beki, Samweli Onditi Kwa mkataba wa miaka 2 Kutoka Kagera Sugar FC.
✅Klabu ya Mtibwa Sugar imekamilisha Usajili wa Kocha, Mecky Mexime Kutoka Dodoma Jiji FC.
✅Klabu ya Young Africans imekamilisha Usajili wa beki wa Kushoto, Mohamed Hussein Kwa Mkataba wa Miaka, Kutoka Simba SC kama Mchezaji huru.
✅Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha usajili wa beki wa kati Vedastus Masinde mwenye Umri wa miaka 19 kutoka TMA FC inayoshiriki Championship.
✅Klabu ya Namungo FC imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji Abdulaziz Shahame “Haaland” kwa mkataba wa miaka miwili Kutoka TMA FC.
✅Klabu ya Tabora United imekamilisha
usajili wa kiungo wa kati Palai Mba Manjie raia wa Cameroon mwenye Umri wa miaka 24 Kutoka Victoria United ya Nigeria.
✅Lucas Kikoti amejiunga na Namungo FC akitokea Coatal Union FC Kwa mkataba wa mwaka mmoja.
✅Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kiungo Mshambuliaji Morice Abraham mwenye Umri wa miaka 21 kama Mchezaji huru Kutoka FK Spartak Subotica ya Serbia.
✅Klabu ya JKT Tanzania imekamilisha Usajili wa golikipa, Ramadhan Chalamanda Kwa mkataba wa miaka 2 Kutoka Kagera Sugar FC
✅Klabu ya Mbeya City imekamilisha usajili wa kiungo, Sospeter Bajana kama Mchezaji huru Kutoka Azam FC.
✅Klabu ya Simba wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Al Hilal Raia wa Mauritania, Khadim Diaw mwenye Umri wa miaka 27.
✅Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha Usajili wa beki, Kelvin Kijili Kwa Mkataba wa Miaka Miwili kama Mchezaji huru.
✅Mshambuliaji wa zamani wa Horoya na Young Africans, Heritier Ebenezer Makambo mwenye Umri wa miaka 31 amejiunga rasmi na Namungo FC ya Lindi kwa miaka miwili kutoka Tabora United FC.
✅Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa winga hatari wa Ivory Coast, Mofossé Karidioula mwenye Umri wa miaka 27 Kutoka Haras El Hodoud ya Misri.
✅Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Muhsini Malima Makame mwenye Umri wa 24 kutoka Zed FC tangu ya Misri.
✅Mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda hatokuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao wa 2025/2026 baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu.
✅Kiungo Mzamiru Yassin hatokuwa sehemu ya kikosi Cha Simba sc msimu ujao wa 2025/2026 baada ya mkataba wake na Simba sc kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.
✅Klabu ya Yanga SC ipo katika hatua za mwisho mwisho za kukamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji, Offen Chikola mwenye Umri wa miaka 26 kutoka Tabora Utd Kwa mkataba wa miaka miwili.
✅Klabu ya Young Africans imefanya Mawasiliano na Kiungo Mshambuliaji, Gibril Sillah Sillah raia wa Gambia mwenye Umri wa miaka 26 ambaye yupo huru baada ya kumalizana na Azam FC kwaajili ya kuwatumikia Wananchi hao Msimu ujao wa 2025/2026.
✅Klabu ya Singida Black Stars inakaribia kukamilisha usajili wa golikipa wa Simba, Hussein Abel Kama mchezaji huru.
✅Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Golikipa, Aishi Salum Manula Mwenye Umri wa Miaka 29 Kwa Mkataba wa Miaka Miwili kutoka Simba SC kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Simba Kumalizika.
✅Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa mlinzi, Lameck Lawi Kutoka Coastal Union ya mkoani Tanga.
✅Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa Kiungo mkabaji, Abdulnassir Mohammed Abdallah Kutoka Mlandege FC kwa mkataba wa miaka mitatu.
✅Klabu ya Tabora United ipo kwenye hatua za mwisho Kukamilisha Usajili wa Golikipa wa timu ya Taifa ya Ghana, Frederick Asare mwenye Umri wa miaka 26 Kutoka Asante Koto kama Mchezaji huru
✅Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Andrew Simchimba Kutoka Geita Gold FC.
Mashambaliaji huyo wa zamani wa vilabu vya KMC, Azam Fc na Ihefu Fc msimu uliopita alifanukiwa kufunga jumla ya Mabao 18 ya NBC Championship.
✅Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa aliyewahi kuwa kocha wa Tabora United, Anicet kiazayidi ikiipiku coastal Unioni baada ya kuweka donge nono zaidi yao.
✅Klabu ya Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma imekamilisha Usajili wa aliyekuwa Mlinzi wa Kati wa Kagera Sugar FC ya Kagera, Mohamed Mussa Kwa Mkataba wa miaka miwili.
✅Klabu ya Singida Black Stars imekamilisha Usajili wa aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Klabu Yanga, Miguel Gamondi Kwa mkataba wa mwaka mmoja.
✅Klabu ya Pamba Jiji FC Imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Abdallah Idd Pina kutoka Mlandege FC ya Zanzibar Kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mlandege FC.
✅Klabu ya Ismaily Sc ya Misri imekamilisha Usajili wa aliyekuwa kocha wa Yanga Sc, Miloud Hamdi kama Kocha Mkuu.
✅Klabu ya Azam FC imekamilisha Usajili wa Kocha, Florent Ibenge mwenye Umri wa miaka 63 Kutoka Al Hilal SC ya Sudan.
✅Klabu ya Hassania d’Agadir ya Morocco ipo kwenye hatua za mwisho Kukamilisha Usajili wa aliyekuwa Kiungo mkabaji wa Simba SC, Fabric Ngoma mwenye Umri wa miaka 31.
✅Klabu ya Young Africans imekamilisha uhamisho wa Mchezaji Aboubakar Nidhar Othman (Ninju ) aliyekuwa kwa mkopo JKU SC ya Zanznibar akitokea timu ya vijana ya Azam FC, Ninju (17).
✅Mshambuliaji Cyprian Kipenye na Kiungo Morice Abraham ni majina pekee aliyoyapitisha Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba SC, Fadlu Davies baada ya kuwafuatilia kwenye majaribio klabuni hapo.
✅Uongozi wa klabu ya Young Africans umeachana na kiungo aliyekuwa anaitumikia Klabu hiyo kwa mkopo akitokea Singida Black Stars Aziz Andambwile baada ya mkataba wake kuisha.
✅Wengine ni Kennedy Musonda ambaye tayari ameshaondoka nchini Tanzania, Wakati Winga wao Jonathan Ikangolombo akiwa kwenye mazungumzo juu ya hatma yake ya kutolewa kwa mkopo ama kuvunjwa kwa kandarasi yake
✅Mlinda lango, Abubakar Khomeiny pia nae hatokuwa sehemu ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2025/2026.
✅Klabu ya Azam Imekamilisha Usajili wa Kiungo Mkabaji, Himid Mao mwenye Umri wa miaka 32 kutoka Ghazl El Mahalla ya Misri.
✅Klabu ya Mbeya City imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Dickson Ambundo Kutoka Fountain Gate FC kama Mchezaji huru
✅Klabu ya Namungo Fc wapo kwenye Mazungumzo na beki Hamza Better Kutoka TMA FC NBC Championship.
Tetesi Zaidi na Usajili Uliokamilika Dirisha Kubwa la Usajili 2025/2026 Bofya HAPA

Natafuta ajira