NAFASI 114 Za Kazi Chemba District Council

Filed in Ajira by on 22.07.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI 114 Za Kazi Chemba District Council

NAFASI 114 Za Kazi Chemba District Council

NAFASI 114 Za Kazi Chemba District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA WAKUSANYA MAPATO VIJIJINI – NAFASI 114 REVENUE COLLECTORS

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba anawatangazia Wananchi wote wenye sifa, nafasi 114 kazi ya kukusanya mapato kama ifuatavyo:-

SIFA ZA MUOMBAJI:

  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
  • Awe na elimu kuanzia Darasa la Saba na kuendelea.
  • Awe ni mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
  • Awe na mdhamini atakaye mdhamini wakati wa
    kujaza mkataba (mke, mume, baba, mama au mtu yeyote mwenye mali isiyo hamishika kama vile shamba, nyumba n.k).
  • Awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai au kuhukumiwa kifungo jela katika Mahakama yoyote.
  • Awe tayari kufanya kazi katika eneo lolote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
  • Yeyote aliyewahi kufanya kazi Halmashauri na kuisababishia hasara au upotevu wa mapato au kudaiwa na Halmashauri, HARUHUSIWI KUOMBA KAZI HII.
  • Awe na namba ya NIDA itakayo tumika wakati wa usajili wa Mkusanya Mapato.

MASHARTI YA KUOMBA:

  • Barua ya maombi ipitie kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji au Kata.
  • Barua iambatane na picha ya muombaji na mdhamini wake zilizo pigwa siku za karibuni.

MAJUKUMU YA MKUSANYA MAPATO.

  • Kukusanya mapato ya Halmashauri kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyopo katika eneo la Wilaya ya Chemba atakalopangiwa kufanya kazi kwa kutumia mashine ya Kielektroniki (POS).
  • Kuwasilisha benki kupitia akaunti ya mapato ya Halmashauri makusanyo yote yaliyokusanywa kwa wakati katika siku za kazi au siku ya kwanza ya kazi ya wiki au baada ya sikukuu.
  • Kutoa risiti za Mashine ya Kielektroniki (POS) kiasi sawa na fedha atakayopokea kutoka kwa mlipaji.
  • Kutunza vifaa vya kukusanyia mapato (POS, Rejista) na Nyaraka za benki au Halmashauri zinazothibitisha uingizaji wa fedha benki.
  • Kufanya uhakiki kila siku wa makusanyo ya siku na taarifa ya mashine ya kukusanyia mapato na kuiwasilisha.
  • Kuwasilisha Halmashauri mashine ya kukusanyia mapato (POS) kwaajili ya Ukaguzi /uchunguzi na.
  • Kufanya kazi nyingine zinazohusu mapato kwa kadri atakavyoelekezwa na Mwajiri.

MUDA/ MASHARTI YA AJIRA.

  • Ajira hii ni ya Mkataba wa miezi sita kuanzia mwezi Agosti 2025 hadi Januari 2026.
  • Atakuwa chini ya uangalizi wa Mtendaji wa Kata na Kijiji husika na.
  • Mkusanyaji ataongezewa mkataba kutokana na juhudi yake katika ukusanyaji wa mapato.

MALIPO YA MKUSANYA MAPATO
Malipo kwa kazi ya ukusanyaji mapato yatakuwa ni asilimia 5 (5%) ya mapato aliyokusanya na kuyawasilisha Benki kwa wakati

Maombi yatumwe ifikapo au kabla ya tarehe 28 Julai, 2025 kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S. L. P. 830,
CHEMBA.

Mwisho wa Kituma Maombi ni tarehe 28 Julai 2025 saa 9.30 mchana.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *