MAJINA 517 ya Walioitwa Kazini Kada ya Afya Kupitia Programu ya TIMCHIP

Filed in Kuitwa Kazini by on 23.07.2025 0 Comments
Share This Post
MAJINA 517 ya Walioitwa Kazini Kada ya Afya Kupitia Programu ya TIMCHIP

MAJINA 517 ya Walioitwa Kazini Kada ya Afya Kupitia Programu ya TIMCHIP

MAJINA 517 ya Walioitwa Kazini Kada ya Afya Kupitia Programu ya TIMCHIP

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji wote wa kazi za mkataba katika Programu ya Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto nchini Tanzania yaani Tanzania Maternal and Child Health Investment Program (TMCHIP) kwa nafasi mbalimbali za kada za afya waliowasilisha maombi ya ajira katika kipindi cha mwezi wa Desemba, 2024 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika hivyo waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika Halmashauri walizopangiwa.

Ajira hizi ni za mkataba wa miaka miwili (miezi ishirini na nne).

Waombaji wote waliopata nafasi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
  • Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku kumi na nne (14) nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka iwezekanavyo.
  • Kuwasilisha Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma kwaajili yankuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
  • Waombaji waliopata nafasi za ajira watakaoripoti bila ya kuwa na Vyeti Halisi (Original Certificates) vya Kidato cha Nne, Kidato Sita, Chuo Kikuu, NACTE na vyeti halisi vya usajili wa mabaraza ya kitaaluma hawatapokelewa.
  • Waombaji waliopata nafasi za ajira wanajulishwa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kubadilisha vituo vya kazi walivyopangiwa na wanakumbushwa kuwa ajira hizi ni
    za mkataba.
  • Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili, watambue kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi
    zitakapotangazwa.
  • Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia Mafunzo Elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.

Orodha ya majina ya waombaji waliopangiwa vituo vya kazi imeambatishwa hapa chini kwenye PDF.

ORODHA YA WAAJIRIWA WA KADA YA AFYA KUPITIA PROGRAMU YA TIMCHIP

Tangazo Limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI,
Mji wa Serikali – Mtumba,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
23 Julai, 2025

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *