SIFA Za Kupata Ufadhili wa Masomo Samia Scholarship 2025/2026

Filed in Elimu by on 23.07.2025 0 Comments
Share This Post
SIFA Za Kupata Ufadhili wa Masomo Samia Scholarship 2025/2026

SIFA Za Kupata Ufadhili wa Masomo Samia Scholarship 2025/2026

SIFA Za Kupata Ufadhili wa Masomo Samia Scholarship 2025/2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza Programu ya Ufadhili iitwayo ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ kwa masomo ya shahada ya awali kwa wanafunzi 1,050 na wanafunzi 51 wenye mahitaji maalumu waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya taifa ya kidato cha sita inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika tahasusi za sayansi (PCB, PCM, CBG, PGM, CBA, PMC na CBN).

Ufadhili wa ‘SAMIA SCHOLARSHIP’ utagharimia masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi hao ambao wameomba au kupata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba kwa kuzingatia Mwongozo’ uliotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambayo inasimamia utekelezaji wa ‘Scholarship’ hizi.

Mwongozo huo unapatikana www.heslb.go.tz

Aidha ni lazima kila mwombaji ambaye amekidhi Vigezo vya Kuomba Samia Scholarship 2025/2026 awe na sifa zilizoanishwa hapa chini.

Mwombaji wa Ufadhili wa Masomo Samia Scholarship 2025/2026 lazima awe;

  • Awe Mtanzania.
  • Awe na ufaulu wa juu (Daraja la kwanza, pointi 3 hadi 5) kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2025 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika tahasusi za sayansi zilizotajwa.
  • Awe amepata udahili katika Chuo cha Elimu ya Juu hapa nchini
    kinachotambuliwa na Serikali katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Sayansi za Tiba ambazo zimetajwa katika kundi la kwanza (Cluster 1) katika Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Wanafunzi wa Shahada za Awali
    kwa mwaka wa masomo 2025/2026 unaopatikana www.heslb.go.tz.
  • Awe ameomba ufadhili kwa usahihi kwa njia iliyoelekezwa.
  • Lazima awe miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwaajili ya kunufaika na ‘Scholarship’.

Aidha Ufadhili huu utazingatia viwango na miongozo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya kugharimia maeneo yafuatayo;

  • Ada ya Mafunzo.
  • Posho ya Chakula na Malazi.
  • Posho ya Vitabu na Viandikwa.
  • Mahitaji Maalumu ya Vitivo.
  • Mafunzo kwa Vitendo
  • Utafiti.
  • Vifaa Saidizi kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalumu.
  • Bima ya Afya

Pia Kwa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo kupitia ufadhili huu, ili kusoma shahada za awali watagharimiwa kwa muda wa kati ya miaka mitatu hadi mitano kulingana na programu husika walizodahiliwa.

SOMA ZAIDI TAARIFA HII HAPA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *