NAFASI 10 Za Kazi Opareta wa Compyuta Msaidizi II MDAs & LGAs

Filed in Ajira by on 10.08.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI 10 Za Kazi Opareta wa Compyuta Msaidizi II MDAs & LGAs

NAFASI 10 Za Kazi Opareta wa Compyuta Msaidizi II MDAs & LGAs

NAFASI 10 Za Kazi Opareta wa Compyuta Msaidizi II MDAs & LGAs

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅OPARETA WA COMPYUTA MSAIDIZI II (ASSISTANT COMPUTER OPERATOR)
NAFASI – 10

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kutunza kumbukumbu za shughuli za kila siku.
  • Kugundua na kusahihisha makosa yanayotokea katika data.
  • Kufanya kazi za Kompyuta.
  • Kuchapa orodha ya makosa.
  • Kufanya programu ya matumizi.
  • Kuchapa taarifa za mwisho na
  • Kufanya kazi chini ya usimamizi wa Opereta wa Kompyuta Daraja la II.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliomaliza kidato cha nne (IV) wenye Astashahada ya mwaka mmoja ya masomo ya awali ya Kompyuta yanayojumuisha Uendeshaji wa Kompyuta wa Msingi (Basic computer operations), Progam Endeshi (Operating system), na Program Tumizi (Application Programs) au Fundi Sanifu wa Kompyuta kutoka Kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanaambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajili ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti.
  • vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
  • Computer Certificate.
  • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’) (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 22 Agosti 2025

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *