NAFASI 18 Za Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 18 Za Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
NAFASI 18 Za Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
✅AFISA MAENDELEO YA MICHEZO MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISSTANT GAME AND SPORTS DEVELOPMENT OFFICER II) – NAFASI 18
MAJUKUMU YA KAZI
- Kufundisha fani mbalimbali za michezo katika eneo lake la kazi.
- Kukusanya takwimu mbalimbali za sekta ya michezo katika eneo lake la kazi.
- Kusaidia kutambua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa watoto katika eneo lake
la kazi. - Kushauri namna ya uendeshaji wa vyama na vilabu vya michezo katika eneo lake la kazi kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
- Kusaidia kuendeleza fani ya michezo ya jadi katika eneo lake la kazi.
- Kushauri kuhusu uendeshaji wa miundombinu ya michezo katika eneo lake la kazi.
- Kusaidia kuhamasisha michezo kwa wote katika eneo lake la kazi
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Astashada ya Elimu ya Michezo (Physical Education),sayansi ya michezo (certificate in sports science), uongozi na utawala wa michezo (sports
management and administration), Elimu ya michezo (Sports coaching and Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi ya Mshahara wa Serikali yaani TGS B.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita ambaye amefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na kufaulu mafunzo ya Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili (2) yenye somo la kufundishia la Fasihi ya Kiingereza
(English Literature) kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulIka na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGTS- C.
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
- Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanaambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajili ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti.
- vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate.
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’) (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 22 Agosti 2025
Tags: NAFASI 18 Za Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
