NAFASI 20 Za Mpishi Daraja la Pili II MDAs & LGAs

NAFASI 20 Za Mpishi Daraja la Pili II MDAs & LGAs
NAFASI 20 Za Mpishi Daraja la Pili II MDAs & LGAs
✅MPISHI DARAJA LA PILI II (COOK II) – NAFASI 20
MAJUKUMU YA KAZI
- Kupika vyakula vya aina mbalimbali.
- Kutayarisha orodha ya vyakula vya mlo kamili (Balanced Diet).
- Kuhakikisha vyombo vya kupikia vyakula vinakuwa safi na
- Kufanya kazi nyingine atakazoagizwa na Msimamizi wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika fani ya “Food Production” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
- Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanaambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajili ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti.
- vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate.
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’) (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 22 Agosti 2025
