MAGAZETI ya Leo Jumatano 03 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 03 September 2025
MAGAZETI ya Leo Jumatano 03 September 2025

Serikali ya Kijeshi ya Taifa la Burkina Faso imepitisha kwa kauli moja sheria inayopiga marufuku mapenzi ya jinsia moja ikiwa ni sehemu ya mageuzi ya sheria za Familia na Uraia ambapo sheria hii mpya iliyopitishwa Septemba 1 2025 na Bunge la mpito lenye Wajumbe 71 wasiochaguliwa, inatoa adhabu ya kifungo cha miaka miwili hadi mitano jela pamoja na faini kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Waziri wa Sheria wa Burkina Faso, Edasso Rodrigue Bayala amesema kuwa kama Mtu atabainika kushiriki vitendo hivyo au vitendo vinavyofanana na hivyo atafikishwa mbele ya Hakimu lakini pia Wageni watakaobainika na makosa hayo watafukuzwa nchini humo mara moja.
Hatua hii inaifanya Burkina Faso kuungana na zaidi ya nchi 30 za Afrika ambazo tayari zimeweka marufuku ya kisheria dhidi ya mapenzi ya jinsia moja ambapo nchi jirani Mali ilipitisha sheria kama hiyo mwezi Novemba 2024, nchi nyingine kama Ghana na Uganda pia zimeimarisha sheria zao kali licha ya kukosolewa vikali Kimataifa.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
