NAFASI 22 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba-Kagera

Filed in Ajira by on 09.09.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI 22 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba-Kagera

NAFASI 22 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba-Kagera

NAFASI 22 Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba-Kagera

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, anawaalika Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya kazi 22 za mkataba katika nafasi zifuatazo:-

✅AFISA TEHAMA – NAFASI 2

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe mwenye Shahada katika fani ya TEHAMA kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali mwenye uzoefu walau mwaka mmoja katika ‘Data Entry’

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kuingiza kwa uharaka na kwa usahihi takwimu za kitabibu, kimaabara na fomu nyinginezo katika hifadhidata (Data base).
  • Kuchambua na kutunza takwimu/data katika mpangilio wa namba au tarehe Kuwasiliana na msimamizi wa kazi kuhusiana na fomu zenye tatizo.
  • Kuwasiliana na msimamizi wa kazi kuhusiana na matatizo ya hifadhidata.
  • Kufanya upatanisho (Reconciliation) baina ya hifadhidata zinazotofautiana.
  • Kutoa ushauri namna nzuri ya uboreshaji wa takwimu/taarifa na utunzaji wake.
  • Kushughulikia matatizo ya kitehama inapobidi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU – AFYA – NAFASI 6

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe mwenye elimu ya kidato cha nne na Stashahada katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu za Afya kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kupokea wagonjwa na kuwasajili kwenye vitabu vya mapokezi.
  • Kuwafungulia wagonjwa majalada.
  • Kutunza majalada ya wagonjwa na kumbukumbu zinazohusu wagonjwa.
  • Kukusanya, kutunza, kuchambua na kutafsiri taarifa za Afya na zile zinazohusiana na Afya.
  • Kuandaa taarifa za Afya za Hospitali na kuziingiza kwenye mfumo wa taarifa.
  • Kuhakiki/kusimamia ubora wa takwimu za wagonjwa.
  • Kuandaa taarifa zote za Afya zinazohitajika katika ngazi ya Hospitali, Wizara n.k. na kuziwasilisha kwa Mganga Mfawidhi.
  • Kusimamia utendaji wa kazi watumishi waliochini yako,
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II – NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe na elimu ya kidato cha nne na Stashahada ya Uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania na mwenye

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kutoa huduma za Uuguzi.
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakaopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅MTEKNOLOJIA MIONZI DARAJA II NAFASI 4

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na cheti cha kidato cha nne, Stashahada katika fani ya Mteknolojia Mionzi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Baraza husika.

MAJUKUMU

  • Kuwapima wagonjwa wanaoelekezwa kwenye eneo lake la kazi.
  • Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi.
  • Kukagua picha za X-Ray zilizopimwa kwa ubora na kutosheleza (Diagnostic quality).
  • Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia madaktari waliowatuma wagonjwa
  • Kusimamia watumishi walio chini yake.
  • Kutoa ushauri kuhusu masuala ya kazi za Radiolojia na Mionzi katika eneo lake la kazi.
  • Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (sterilization).
  • Kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wanaopangiwa kazi katika eneo lake la kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

✅MSAIDIZI WA AFYA – NAFASI 5

SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe mwenye elimu ya kidato cha nne na Astashahada katika fani yake kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kufanya usafi wa vifaa vya kazi, usafi wa wodi na mazingira.
  • Kusaidia wagonjwa wenye ulemavu na wasiojiweza katika kwenda haja
    (kubwa na ndogo na kuoga).
  • Kumsaidia kumlisha mgonjwa asiyejiweza.
  • Kuchukua nguo za mgonjwa kuzipeleka kwenda kufuliwa.
  • Kuchukua sampuli za mgonjwa kwa ajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu.
  • Kutayarisha vifaa kwa ajili ya kusafisha na kufunga majeraha.
  • Kufuatilia mahitaji ya dawa kwa wagonjwa kutoka hifadhi ya dawa.
  • Kufanya shughuli nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi.

✅MPISHI II NAFASI 1
Awe mwenye Cheti cha kidato cha nne aliyefuzu mafunzo katika fani ya Mapishi kutoka katika vyuo vinavyotambulika na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kufanya uchambuzi wa vyakula kulingana na wahitaji.
  • Kutoa taarifa kwa Msimamizi kama kuna upungufu wa chakula au ongezeko la mhitaji ili suala hilo lishughulikiwe haraka.
  • Kutunza vifaa vyote vinavyohusika na kazi za mapishi.
  • Kufanya usafi wa chumba cha kupikia pamoja na vyombo vya kupikia.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

MASHARTI YA KAZI

  • Ajira itakuwa ni ya mkataba wa mwaka mmoja.
  • Baada ya kipindi cha mkataba kuisha, Mfanyakazi atakayekuwa ameonesha ufanisi katika utendaji mkataba wake utaweza kuhuishwa.

Mambo ya kuzingatia kwa waombaji

  • Awe ni Mtanzania
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makosa ya jinai
  • Awe hajawahi kufukuzwa/ kupunguzwa toka Serikalini.
  • Awe na Umri kuanzia miaka 18 hadi 45

Barua zote za maombi ziambatishwe na vivuli vya vyeti vya kuzaliwa, kitambulisho cha uraia, vyeti vya elimu na ujuzi, Maelezo binafsi (CV) yaliyoambatana na wadhamini wawili, leseni hai pamoja na picha moja (1) ya rangi (Passport size).

MAOMBI YOTE YATUMWE KWA
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, S.L.P 265,
BUKOBA.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 19/09/2025 saa 9:00 alasiri.

DONWLOAD PDF YA TANGAZO HAPA

JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA


Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *