MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 14 September 2025

MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 14 September 2025
MAGAZETI ya Leo Jumapili tarehe 14 September 2025

Uongozi wa klabu ya Simba leo umekutana na wachezaji na benchi la Ufundi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumanne kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Ally Mangungu kwa pamoja na Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Wakurugenzi, Crestentius John Magori.
Kikao hicho kinafanyika siku tatu baada ya tamasha la Simba Day, klabu ikitambulisha kikosi chake kamili cha msimu mpya na kucheza mechi ya kirafiki dhidi y Gor Mahia ya Kenya ambayo walishinda 2-0.
Taarifa ya Simba juu ya kikao hicho imesema ni kupanga mikakati ya msimu ambao watauanza Jumanne kwa mchezo dhidi ya Yanga.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Yanga nayo imekutana makao makuu ya klabu hiyo, Jangwani, Dar es Salaam kujadili mradi wa ujenzi wa Uwanja.
Kikao hicho kimefanyika siku moja tu baada ya uongozi huo kukabidhiwa Hati ya kiwanja chao wanachotaka kuwekeza mradi huo kilichopo eneo la Jangwani, jirani na makao makuu ya klabu hiyo.
Makamu wa Rais wa klabu, Arafat Haji na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Gulamali hawakuhudhuria kikao hicho, lakini wakishiriki kwa njia ya mtandao.
Ikumbukwe jana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius John Ndejembi alikabidhi Hati ya kiwanja cha klabu hiyo wakati wa tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
