NAFASI Za Kazi Arusha City Council

NAFASI Za Kazi Arusha City Council
NAFASI Za Kazi Arusha City Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi katika Halmashauri hii baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchanganuo ufuatao:-
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (06) – INARUDIWA
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari
(Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali yaani TGS B1
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini
(Referees) watatu wa kuaminika. - Waombaji kazi wa kada ya Dereva Daraja la II wenye leseni daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika ya leseni E au C.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, Kidato
cha Nne/Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - “Testimonial”, “Provision Result”, “Statement of Result”, Hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM FOUR and FORM SIX RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafu katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji wa kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CCA. 45/257/01/D wa tarehe 30 Novemba, 2010
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira, ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji kazi wenye majina tofauti wawe na hati ya kiapo (DEED POL).
- Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waombaji kazi watakaopata nafasi ya kuitwa kwenye usaili wanashauriwa kuja na mavazi yanayozuia baridi kutokana na hali ya hewa ya Jiji la Arusha kwa kipindi hiki.
MUHIMU: Kumbuka kutuma barua yako iliyosainiwa pamoja na vyeti kwenda kwa;
Mkurugenzi wa Jiji
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S. L. P 3013
20 Barabara ya Boma
23101 ARUSHA
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kieletroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal).
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA TANGAZO
Mwisho wa kutuma Maombi ya Kazi ni tarehe 20 Oktoba, 2025.
