MASWALI ya Usaili Kusimamia Uchaguzi Mkuu 2025

MASWALI ya Usaili Kusimamia Uchaguzi Mkuu 2025
MASWALI ya Usaili Kusimamia Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa madhumuni ya uendeshaji wa uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia
masharti ya kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge
na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kikisomwa pamoja na kanuni ya 11
ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025,
Msimamizi wa Uchaguzi anawatangazia
waombaji nafasi za Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga Kura, Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya kupigia Kura na Makarani Waongozaji Wapiga Kura kufika kwenye usaili Kwa tarehe tajwa.
Kuelekea Usaili huo, haya ni baadhi ya maswali ya usaili kwa wale walioomba kazi au nafasi ya kusimamia Uchaguzi Mkuu 2025 kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Haya hapa ni Maswali ya Maandishi (Written Interview)
- Eleza majukumu ya Msimamizi/Msimamizi Msaidizi wa Kituo cha Kupigia Kura.
- Taja hatua kuu za mchakato wa upigaji kura siku ya uchaguzi.
- Ni vitu gani vinapaswa kuwepo kwenye kituo cha kupigia kura kabla ya kuanza kazi?
- Eleza hatua za kuhesabu kura na kuwasilisha matokeo.
- Taja changamoto zinazoweza kujitokeza siku ya uchaguzi na jinsi ya kukabiliana nazo.
- Eleza umuhimu wa kutunza siri na uadilifu katika kazi ya uchaguzi.
Haya hapa ni Maswali ya ana kwa ana (Oral Interview)
- Jieleze kwa kifupi na eleza kwa nini unataka kusimamia uchaguzi.
- Ukikuta mpiga kura ana kitambulisho halali lakini jina halipo kwenye daftari, utafanyaje?
- Utafanyaje iwapo kutatokea vurugu au vurugu ndogo kituoni?
- Ungezuiaje wizi au hujuma ya kura kituoni?
- Je, una uzoefu wowote uliowahi kuhusika na uchaguzi kabla? Eleza.
- Kwa nini uadilifu ni muhimu kwa msimamizi wa uchaguzi?
- Ungeelezaje tofauti kati ya msaidizi wa kituo na msimamizi wa kituo?
Maswali yaliyoulizwa Kwa wasailiwa wa Kusimamia Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025.
- Taja majina matatu ya Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. - Taja kazi/majukumu matano (0s) ya kati uliyoomba
- Taja majina kamili (03) ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Vyama Vitatu (03) unajua walioteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kugombea nafasi ya Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
- Taja Sifa nne (04) za Mpiga Kura.
- Taja kirefu cha Chama cha AAFP.
- Taja sifa nne (04) za mgombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Tanzania Bara kuna Vyama vingapi vya Siasa vilivyo sajiliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania na kuruhusiwa kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
- Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utafanyika tarehe…………mwezi wa……
- Fafanua maana na matumizi ya rangi za mifuniko ya masanduku ya kupigia kura (Kura za nafasi ipi zinawekwa kwenye sanduku lenye rangi ipi?)
- A. Rangi nyeusi..
- C. rangi nyeupe..
- B. rangi ya bluu………
2.Taja sifa tano (5) za Watendaji wa vituo wa kusimamia upigaji kura kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 (Maksi 25)
i).
ii).
iii).
iv).
iv).
2.Ikitokea ukapata changamoto katika kituo chako cha kazi wakati wa upigaji Kura utatoa taarifa kwa nani? (Maksi 25)
3.Taja watu watano (5) wanaoruhisiwa kuingia kwenye kituo cha kupigia Kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 2024. (Maksi 25)
i).
ii).
iii).
iv).
v).
4.Taja makundi matano (5) ya viongozi wanaopatikana kupitia Uchaguzi Mkuu unaosimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania. (Maksi 25).
1.Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unahusisha nafasi zipi? (15%)
- A.Mwenyekiti wa kijiji, Diwani na Rais.
- B.Rais, Mbunge na Diwani.
- C.Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji na Wajumbe
2.Uchaguzi Mkuu unafanyika mara ngapi katika kipindi cha miaka mitano? (15%)
- A. Mara moja.
- B. Mara tano.
- C. Kila mwaka
3.Umri wa mwananchi kupiga kura ni…. (15%)
- A. Miaka 40
- B. Miaka 21
- C. Miaka 18
4.Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu utafanyika lini? (15%)
- A. 25/10/2025
- B. 28/10/2025
- C. 29/10/2025
5.Taja vifaa vinne (4) na kazi zake vinavyotumika wakati wa kupiga kura. (40%)
Majibu ya Maswali yaliyoulizwa Kwa wasailiwa wa Kusimamia Uchaguzi Mkuu.
1.Taja rangi za maboksi ya kupigia kura.
- Bluu-Rais
- Nyeusi – Wabunge
- Nyeupe – Madiwani
2.Taja sifa 5 za watendaji wa vituo vya kupigia kura.
- Raia wa Tanzania
- Elimu angalau ya kidato cha nne
- Uaminifu na uadilifu
- Kutokuwa mwanachama hai wa chama cha siasa.
- Kufanya kazi kwa nidhamu na kufuata maelekezo ya NEC.
3 Ikitokea changamoto kituoni wakati wa upigaji kura utatoa taarifa kwa nani?
- IKwa Msimamizi wa kituo cha kupigia kura.
- Kisha kwa Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.
- Halafu kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama changamoto ni kubwa.
4.Taja watu 5 wanaoruhusiwa kuingia kwenye kituo cha kupigia kura.
- Wasimamizi wa kituo cha kupigia kura.
- Mpiga kura aliyesajiliwa katika kituo hicho.
- Mawakala wa vyama vya siasa.
- Askari wa usalama aliyepewa jukumu.
- Waangalizi wa uchaguzi waliothibitishwa na NEC.
5.Taja Makundi 5 ya viongozi wanaopatikana kupitia uchaguzi mkuu.
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Wabunge.
- Madiwani
- Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri (kupitia madiwani).
- Wawakilishi wa viti maalum.
Maswali ya Usaili Kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
1.Eleza kwa kifupi lengo la Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29
Oktoba, 2025.
2.Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ni uchaguzi wa ngapi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi?
3.Ni hatua gani utazichukua kuhakikisha wapiga kura wanapata haki sawa ya kupiga kura bila upendeleo?
(1)
(2)
(3)
4.Eleza wajibu wa wahusika wafuatao katika kituo cha kupigia kura (a)Msimamizi wa Kituo
(b)Msimamizi Msaidizi
(c)Karani…..
(d)Askari
