NAFASI 1588 Za Msaidizi wa Afya Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 1588 Za Msaidizi wa Afya Daraja la II MDAs & LGAs
NAFASI 1588 Za Msaidizi wa Afya Daraja la II MDAs & LGAs
✅MSAIDIZI WA AFYA DARAJA LA II (HEALTH ASSISTANT GRADE II) – Nafasi
1588
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchukua Sampuli za Maji na Chakula na kuzipeleka kwa afisa afya mazingira au afisa afya mazingira msaidizi.
- Kutambua na kuweka kumbukumbu ya vyanzo vya maji.
- Kuandaa ramani ya maeneo yenye uchafuzi wa maji ili kuchukua hatua zinazotakiwa.
- Kushirikiana na kamati za maji za vijiji, na mitaa katika kuhakikisha usalama wa vyanzo vya maji.
- Kuhamasisha jamii kulinda vyanzo vya maji.
- Kuhamasisha jamii kujenga na kutumia vyoo bora.
- Kusaidia kuuelimisha jamii kuhusu tabia njema za usafi.
- Kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa kwa mkuu wake kazi.
- Kuhamasisha jamii kubuni, kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango shirikishi jamii ya afya ya mazingira.
- Kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba.
- Kufanya ukaguzi wa nyumba za kuishi na biashara.
- Udhibiti wa taka hatari zikiwamo taka zitokanazo na huduma za afya.
- Kusimamia sheria ndogondo za afya mazingira na
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha mafunzo ya Msaidizi wa Afya au Fundi Sanifu Afya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: TGHS A
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
Tags: NAFASI 1588 Za Msaidizi wa Afya Daraja la II MDAs & LGAs
