NAFASI 3945 Za Afisa Muuguzi Msaidizi II MDAs & LGAs

Filed in Ajira by on 16.10.2025 0 Comments
Share This Post
NAFASI 3945 Za Afisa Muuguzi Msaidizi II MDAs & LGAs

NAFASI 3945 Za Afisa Muuguzi Msaidizi II MDAs & LGAs

NAFASI 3945 Za Afisa Muuguzi Msaidizi II MDAs & LGAs

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI II (ASSISTANT NURSING OFFICER GRADE II) – Nafasi 3945

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kutoa huduma za uuguzi.
  • Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  • Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
  • Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  • Kutoa huduma za kinga na uzazi; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

NGAZI YA MSHAHARA; TGHS B

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
    watatu wa kuaminika.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
    CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa Kutuma Maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *