NAFASI 381 Za Walimu Daraja la III C Somo la Biashara

NAFASI 381 Za Walimu Daraja la III C Somo la Biashara
NAFASI 381 Za Walimu Daraja la III C Somo la Biashara
✅MWALIMU DARAJA LA III C – SOMO LA BIASHARA (BUSINESS STUDIES) – Nafasi 381
MAJUKUMU YAKAZI
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
- Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
- Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na
unasihi. - Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
- Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule.
- Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biashara au Usimamizi wa Biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration)
AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biashara au usimamizi wa biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: TGTS- D
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha
Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kazi ni tarehe 01 Novemba, 2025.
