MAGAZETI ya Leo Ijumaa 24 October 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 24 October 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 24 October 2025




Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza kuwa Novemba 3, 2025, itachezeshwa droo ya upangaji wa makundi kwa msimu wa 2025-2026 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
Droo hiyo imepangwa kufanyika Johannesburg nchini Afrika Kusini ambapo ile ya Kombe la Shirikisho itaanza saa 8 mchana, wakati Ligi ya Mabingwa ikiwa saa 9 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Wakati ratiba ya droo hiyo ikipangwa, wikiendi hii kuna mechi za marudiano zinachezwa ambapo washindi wa jumla ndiyo watafuzu makundi wakisubiri wapinzani wao wapya.
Katika upangaji wa droo hiyo, CAF itaangalia Viwango vya Klabu vya CAF kwa mwaka 2025 ili kupanga timu kwenye vyungu (pots).
