UFADHILI wa Samia Scholarship Extended\nDS\/ AI+) Fani Za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi 2025/2026

Filed in Elimu by on 09.11.2025 0 Comments
Share This Post

UFADHILI wa Samia Scholarship Extended\nDS\/ AI+) Fani Za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi 2025/2026UFADHILI wa Samia Scholarship Extended\nDS\/ AI+) Fani Za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi 2025/2026

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) inatekeleza programu maalum ya SAMIA EXTENDED
SCHOLARSHIP DS/AI+ inayolenga kuongeza na kukuza ujuzi wa vijana wa
Kitanzania katika fani za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi Shirikishi (Data Science, Artificial Intelligence and Allied Sciences).

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Wizara, kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia inapenda kutangaza fursa
za ufadhili wa masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili kwenye masomo ya
Data Science, Artificial Intelligence, Cybersecurity, Machine Learning na maeneo kama hayo.

MAENEO YA UFADHILI
Ufadhili wa SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP DS/AI+ utajumuisha:

  • Ada ya Mafunzo.
  • Posho ya chakula na malazi.
  • Posho ya vitabu na viandikwa.
  • Mahitaji maalum ya programu (Special Faculty Requirements)
  • Utafiti.
  • Vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu

VYUO VIKUU VINAVYOLENGWA
Ufadhili utatolewa kwa waombaji wenye udahili katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Arusha au Kampasi ya Zanzibar ya India Institutes of Technology (IIT), Madras.

MUDA WA UFADHILI
Wanafunzi watakaofadhiliwa, watagharimiwa kwa kipindi cha miaka miwili ya masomo kuanzia mwaka 2025 kulingana na programu husika walizodahiliwa.

SIFA ZA WAOMBAJI WA UFADHILI
Ufadhili huu utatolewa kwa wanafunzi waliohitimu shahada ya kwanza wenye sifa zifuatazo:

  • Awe Mtanzania.
  • Awe na sifa za kumuwezesha kuajiriwa kama Mkufunzi Msaidizi
    (Tutorial Assistant ) katika Taasisi za Elimu ya Juu za Umma.
  • Muombaji wa ufadhili atatakiwa pia kuomba udahili wa kusoma
    shahada ya Uzamili katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya
    Nelson Mandela au Kampasi ya Zanzibar ya India Institutes of
    Technology (IIT), Madras katika masomo lengwa kama ilivyoanishwa katika kipengele A hapo juu.

MASHARTI YA UFADHILI
Mwanafunzi atakayepata ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP atatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:

  • Awe na udahili katika programu tajwa za masomo katika taasisi
    zilizolengwa.
  • Anapaswa kusoma, kuelewa na kusaini Mkataba wa Makubaliano
    ya Ufadhili wa Masomo kati yake na COSTECH.
  • Anapaswa kuwa na akaunti ya Benki kwa ajili ya fedha atakazolipwa moja kwa moja.
  • Mnufaika hataruhusiwa kubadilisha programu ya masomo aliyopatia ufadhili bila ya idhini ya maandishi kutoka COSTECH.
  • Mnufaika hataruhusiwa kuahirisha masomo, isipokuwa kwa sababu za kiafya na zilizothibitishwa na daktari na kukubalika chuo husika.

Ikiwa mnufaika ataghairi fursa ya ufadhili kabla ya kuanza masomo, atapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwenda kwa:
Mkurugenzi Mkuu,
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
S.L.P 4302
Dar es Salaam, TANZANIA.
Barua pepe: dg@costech.or.tz

UTARATIBU WA KUWASILISHA MAOMBI YA UDAHILI
Maombi ya udahili yawasilishwe kupitia mfumo wa maombi wa Taasisi husika.

MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi udahili yawasilishwe kuanzia tarehe 10 Novemba 2025 hadi 10 Disemba, 2025 kwa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na tarehe 1 Novemba 2025 hadi 24 Novemba 2025 kwa IIT Madras Kampasi ya Zanzibar.

Majina ya watakaopata udahili katika taasisi hizi mbili yatawasilishwa COSTECH na taasisi husika kwaajili ya kufikiriwa kupata ufadhali wa masomo (Scholarship).

Share This Post

Tags: ,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *