MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 November 2025

Filed in Magazetini Leo by on 14.11.2025 0 Comments
Share This Post
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 November 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 November 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 14 November 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Waziri Mkuu mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema Kuwa Serikali yake itasimamia utekelezaji wa mpango mkakati wa ajira milioni nane kwa vijana, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

Akizungumza Alhamisi ya Novemba 13, 2025, bungeni jijini Dodoma wakati akitoa maneno ya shukrani baada ya kuteuliwa kwake, Dk Mwigulu amesema kuwa mpango huo ni sehemu ya ajenda pana ya Serikali ya kuhakikisha vijana wanapata fursa halisi za kiuchumi na kujitegemea.

“Tuna kazi kubwa mbele yetu ya kuhakikisha dira mpya ya maendeleo inakuwa halisi. Hii ni safari ya kuijenga Tanzania yenye uchumi imara, vijana wenye ajira, na wananchi wanaoishi kwa amani,” amesema Dk Mwigulu.

Ameeleza kuwa ajira hizo zitapatikana kupitia miradi ya kimkakati ya Serikali, sekta binafsi na programu za ujasiriamali zitakazowezesha vijana kuunda ajira badala ya kutegemea ajira rasmi pekee.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo utazingatia usawa wa kijinsia na kuhakikisha vijana wa vijijini na mijini wote wananufaika kwa uwiano sawa.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *