MAGAZETI ya Leo Ijumaa 21 November 2025
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 21 November 2025
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ameshinda tuzo ya Mfungaji wa bao bora la mwaka 2025 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Mzize ametangazwa Mshindi wa kipengele hicho katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika Rabat, Morocco Jumatano ya Novemba 19, 2025.
Bao hilo ni lile alilofunga dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025 uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari 4, 2025.
Katika mchezo huo, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mzize ameibuka mshindi mbele ya Abdellah Ouazane, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Barbra Banda, Calvin Fely, Ghizlane Chebbak, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.
