MAGAZETI ya Leo Alhamisi 27 November 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 27 November 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 27 November 2025
Jeshi la Polisi nchini limesema linafanya uchunguzi kuhusu taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kutolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya kwa waandishi wa habari kama ushauri kwa wamiliki wa vituo vya mafuta.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa Jumatano Novemba 26, 2025, uchunguzi huo unalenga kubaini ukweli wa madai hayo, kwani ofisa huyo hana mamlaka ya kuwaita waandishi wa habari na kutoa taarifa rasmi kwao.
Aidha, Polisi wamesema kuwa iwapo itabainika kuwa taarifa hiyo siyo sahihi au ilitolewa kinyume na taratibu, hatua stahiki za kiutumishi na kisheria zitachukuliwa.
Jeshi hilo pia limewataka wananchi kuendelea kupata taarifa sahihi kupitia vyanzo vinavyotambulika kisheria na kuepuka kusambaza taarifa zisizothibitishwa, ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko katika jamii.
