MTAALA Mpya wa Elimu Waanza Rasmi Kidato Cha Nne ni lazima

Filed in Elimu by on 11.12.2025 0 Comments
Share This Post
MTAALA Mpya wa Elimu Waanza Rasmi Kidato Cha Nne ni lazima

MTAALA Mpya wa Elimu Waanza Rasmi Kidato Cha Nne ni lazima

MTAALA Mpya wa Elimu Waanza Rasmi Kidato Cha Nne ni lazima

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda ametangaza mabadiliko ya mtaala mpya wa elimu ambapo amesema kuwa kwa sasa tunaondokana na mtaala wa sasa wa ‘7+4+2+3+’ na kwenda kwenye mtaala mpya wa ‘6+4+2 au 3+3+’ ambao elimu ya msingi itaishia darasa la sita huku elimu ya sekondari kidato cha nne ikiwa ni ya lazima kwa watoto wote na sio hiyari kama ilivyo kwa mfumo huu wa sasa.

Prof. Mkenda ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari hii Disemba 10, 2025 ambapo amesema kuwa Mtaala huo umeanza kufanya kazi kwa darasa la tatu wa sasa na wataishia darasa la sita mwaka 2027 ambapo watafanya mtihani wa majaribio utakao wawezesha kujiunga na kidato cha kwanza.

“Mfumo wetu wa elimu unaweza ukauita ni ‘7+4+2+3+’yaani elimu ya misingi ya miaka saba, Sekondari ya kati miaka minne, sekondari ya juu ya miaka miwili alafu miaka mitatu na kuendelea kwa elimu ya juu kwenda mbele sasa mfumo huu ulianza kutekelezwa hapa nchini kwanzia miaka ya 60, kati ya mwaka 1965 mpaka 1968 mwalimu nyerere aliekeza mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu hapa Tanzania kutoka ule mfumo wa miaka minne kwenda miaka nane mpaka miaka 12 ambayo mtu alikuwa anaweza kusoma miaka minne akawa amemaliza kila kitu”

“Huo ni mfumo ambao tuliurithi kwa mwalimu nyerere, mageuzi makubwa sasa ya mfumo sasa yanakuja kufanyika chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, badala ya ‘7+4+2+3+’ sasa tutakuwa na ‘6+4+2 au 3+3+’ ambayo kwamba kwa mabadiliko haya ambayo nayo tunayatekeleza kwa awamu lakini sisi hatutekelezi kwa awamu Mkoa kwa mkoa tunatekeleza kwa awamu kwa nchi nzima lakini tumeanza mitaala mipya kwanzia darasa la tatu, hawa walioko darasa la tatu 2027 watakuwa wanaishia darasa la sita” Amesema Waziri Wa Eliu Prof. Adolf Mkenda.

SOMA ZAIDI HAPA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *