NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Shahada Za Uzamili nchini Sweden 2025/2026

NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Shahada Za Uzamili nchini Sweden 2025/2026
NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Shahada Za Uzamili nchini Sweden 2025/2026
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden unapenda kuutaarifu umma kuhusu fursa za ufadhili kamili wa masomo ya Shahada ya Uzamili unaotolewa na Taasisi ya Sweden (Swedish Institute – SI).
Ufadhili huu unatolewa katika zaidi ya programu 400 za masomo katika nyanja za utawala, afya ya umma, ujasiriamali na ubunifu, sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati na fani nyinginezo.
Ufadhili huu ni wa malipo ya ada, posho ya kila mwezi pamoja na gharama za usafiri.
Ubalozi unawahamasisha Watanzania wote wenye sifa stahiki kuomba ufadhili
huu.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Awe ameomba au anaomba programu ya Shahada ya Uzamili
inayostahiki kwa udhamini wa SI. - Awe tayari kulipa ada ya maombi ya masomo kupitia mfumo wa udahili wa vyuo vikuu.
- Awe na uzoefu wa kazi unaothibitika.
- Awe na uzoefu wa uongozi kutoka kwa mwajiri wa sasa au wa awali, au kupitia ushiriki katika asasi za kiraia.
UTARATIBU WA MAOMBI
- Kuomba udahili wa chuo kikuu
Mwombaji anatakiwa kutembelea tovuti rasmi ya udahili wa vyuo vikuu vya Sweden kupitia: https://www.universityadmissions.se/intl/start. - Mwombaji aombe chuo na programu ya masomo.
- Tarehe ya mwisho wa maombi ni 15 Januari 2026.
- Kuomba ufadhili wa masomo
Baada ya kupata udahili mwombaji ataomba ufadhili wa masomo kupitia Taasisi ya Sweden (SI) katika tovuti: https://si.se/en/apply/scholar-ships/swedish-institute-scholarships-for-global-professionals/. - Tovuti hii itafunguliwa rasmi tarehe 26 Februari 2026.
Kwa maelezo au ufafanuzi zaidi, wasiliana na Ubalozi kupitia baruapepe: mailbox@tanemb.se.
Tags: NAFASI Za Ufadhili wa Masomo Shahada Za Uzamili nchini Sweden 2025/2026
