MFAHAMU Steven Robert Barker Kocha Mpya wa Simba SC

Filed in Michezo by on 20.12.2025 0 Comments
Share This Post
MFAHAMU Steven Robert Barker Kocha Mpya wa Simba SC

MFAHAMU Steven Robert Barker Kocha Mpya wa Simba SC

MFAHAMU Steven Robert Barker Kocha Mpya wa Simba SC

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Klabu ya Simba SC imetangaza kukamilisha Usajili wa Kocha wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Steven Robert Barker, anayejulikana kama Steve Barker Kutoka Stellenbosch FC kwao Afrika Kusini.

Steven Robert “Steve” Barker ni mchezaji wa zamani wa soka na kocha wa soka wa Afrika Kusini, ambaye sasa ni kocha mkuu wa Stellenbosch Football Club, klabu inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini (Betway Premiership).

Steven Robert Barker alizaliwa Desemba 23, 1967 huko Maseru, Lesotho na ni mjukuu wa kocha maarufu wa Afrika Kusini, Clive Barker inshort ametokea kwenye familia ya soka

Steven Robert Barker akiwa Mchezaji, alicheza katika nafasi ya kiungo kwa vilabu vya Wits University na SuperSport United kabla ya kuachia soka ya kucheza na kuingia uingizaji katika uongozi wa ufundi.

Barker alianza kazi yake ya uongozi akiwa kocha wa University of Pretoria, na aliongoza timu hiyo hadi kupanda daraja la Ligi Kuu ya Afrika Kusini, baadaye alifundisha AmaZulu FC kabla ya kujiunga na Stellenbosch FC mwaka 2017.

Tangu kujiunga na Stellenbosch, amekuwa akijenga timu imara, akiwapeleka Ligi kuu na kuwafanya wapate mafanikio yaliyojulikana, mafanikio yake na Stellenbosch FC.

Aliongoza Stellenbosch FC kupanda kutoka daraja la kwanza hadi Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Msimu wa 2023, timu yake ilishinda Carling Knockout Cup (kombe la ligi kuu), ubingwa mkubwa wa kwanza kwa klabu hiyo.

Stellenbosch pia imefuzu mara kwa mara kwa michuano ya CAF Confederation Cup na kufika hatua za juu, jambo lililoleta sifa kwa kocha Barker.

Steven Robert Barker Kocha Mpya Simba SC

Steven Robert Barker Kocha Mpya Simba SC

Barker amefikia alama muhimu ya kucheza mechi zaidi ya 300 akiwa kocha wa Stellies tangu 2017, ikionyesha utulivu na uongozi wa muda mrefu.

Kwa kifupi, Steve Barker ni mmoja wa makocha wenye uzoefu mkubwa na mafanikio thabiti katika soka la Afrika Kusini, pia ana uzoefu nalo tangu akiwa mchezaji na mpaka kuwa kocha, Steven ni mwalimu kwanza anahitaji kuvumiliwa, kupewa muda kisha awape kilicho bora zaidi.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *