KUITWA Kazini Bunge la Tanzania

KUITWA Kazini Bunge la Tanzania
KUITWA Kazini Bunge la Tanzania
Katibu wa Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Bunge waliotajwa katika Tangazo hili kwamba, walifaulu kushinda waombaji kazi wenzao kwenye usaili uliofanyika tarehe 20 – 23 Disemba, 2025 katika Ofisi za Bunge Dodoma.
Hivyo, wahusika wanaarifiwa kwamba wanatakiwa kuripoti kazini Ofisi ya Bunge Dodoma ifikapo tarehe 05 Januari, 2026 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira zao na kupangiwa kazi.
Waombaji kazi wanaoitwa kuripoti kazini wanatakiwa kufika wakiwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia Kidato cha IV na kuendelea kulingana na sifa za kazi, Cheti cha Kuzaliwa, Kitambulisho cha Taifa, Cheti halisi cha Ndoa (kama ipo); na Vyeti halisi vya kuzaliwa mtoto/watoto (kama wapo).
Kwa ambao masharti ya kazi zao yanawataka kusajiliwa na Mabaraza au Bodi zao za Kitaaluma wanatakiwa kufika wakiwa na vyeti vyao vya usajili pamoja na leseni halali (valid licence) za kufanyia kazi.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?DONWLOAD PDF YA MAJINA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
