MWONGOZO wa kujitolea katika Utumishi wa Umma

MWONGOZO wa kujitolea katika Utumishi wa Umma
MWONGOZO wa kujitolea katika Utumishi wa Umma
Mwongozo wa kujitolea katika Utumishi wa Umma ni nyenzo muhimu inayoweka utaratibu wa kuzingatiwa kwa Taasisi za Umma na Vijana wanaomaliza Vyuo na kuomba nafasi za kujitolea ili kujipatia ujuzi na uzoefu wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali wakati wanasubiri kuajiriwa.
Kwa kipindi chote kumekuwepo na utaratibu usio rasmi wa namna ya kuwapata na kuwasimamia Vijana wanaoomba nafasi za kujitolea katika Utumishi wa Umma.
Suala hili limesababisha Taasisi za Umma kuwa na utaratibu na namna tofauti za kushughulikia masuala
yanayohusu vijana wanaojitolea hivyo kusababisha malalamiko miongoni mwao.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina dhamana ya kutunga na kusimamia Sera na Miongozo mbalimbali inayohusu Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Kutokana na dhamana hii na kwa mujibu wa Kifungu Na. 35A cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298, Ofisi hii imeshirikiana na wadau mbalimbali kuandaa Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma ambao unatoa dira,
mwelekeo, utaratibu na mambo ya kuzingatiwa katika kuwapata na kuwasimamia vijana wa kujitolea kwenye Utumishi wa Umma.
Mwongozo wa Kujitolea katika Utumishi wa Umma unabainisha namna Taasisi za Umma zitakavyowapata na kuwasimamia vijana wa kujitolea ikizingatiwa kuwa vijana hawa si waajiriwa katika Utumishi wa Umma.
Ieleweke kuwa kujitolea kwao si kigezo cha kuajiriwa katika Utumishi wa Umma bali ni kuwajengea uzoefu na ujuzi kupitia fani mbalimbali walizosomea ili kuwawezesha kushindana kwenye soko la ajira la ndani na nje ya nchi na hatimaye kuajiriwa.
Ni matarajio ya Serikali kuwa Mwongozo huu utaweka utaratibu unaofanana kisera na kiutendaji katika kushughulikia masuala ya kujitolea kwenye Taasisi za Umma.
Aidha, utaondoa malalamiko na dhana ya upendeleo iliyopo miongoni mwa wadau na vijana wanaojitolea kwenye Utumishi wa Umma katika fani mbalimbali.
Kwa lengo la kuimarisha Usimamizi na Utawala Bora, ninazielekeza Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
kuzingatia na kuutumia Mwongozo huu ili kufikia azma ya Serikali ya kuwa na utaratibu Maalum wa namna bora ya
kuwapata na kuwasimamia Vijana wanaojitolea na kuweka usawa ili kuongeza wigo wa kujifunza na kupata uzoefu kupitia Taasisi za Umma zinazotoa huduma kwa Wananchi.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?DONWLOAD PDF YA MWONGOZO HAPA
Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
