NAFASI 709 Za Walimu Daraja la III C Somo la Hisabati MDAs & LGAs

Filed in Ajira by on 14.01.2026 0 Comments
Share This Post
NAFASI 709 Za Walimu Daraja la III C Somo la Hisabati MDAs & LGAs

NAFASI 709 Za Walimu Daraja la III C Somo la Hisabati MDAs & LGAs

NAFASI 709 Za Walimu Daraja la III C Somo la Hisabati MDAs & LGAs

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅MWALIMU DARAJA LA III C – HISABATI (MATHEMATICS) – Nafasi 709

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa.
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule na
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Hisabati
    AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Hisabati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: TGTS- D

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.
  • Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi. Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
  • Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa
    kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
    CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
    Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
    kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa ‘GPA’ kutoka TCU.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Januari, 2026.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *