LAURINDO Dilson Maria Aurelio “DEPU” ni Mwananchi

LAURINDO Dilson Maria Aurelio “DEPU” ni Mwananchi
LAURINDO Dilson Maria Aurelio “DEPU” ni Mwananchi
Klabu ya Young Africans imekamilisha Usajili wa mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurelio “DEPU” raia wa Angola Kutoka Radomiak inayoshiriki ligi daraja
la kwanza nchini Poland.
Depu amewahi kuvitumikia vilabu vya Petro de Luanda ya Angola, Gil Vicente ya Ureno na Vojvodina ya Serbia.
Depu pia ameitumikia timu ya Taifa ya Angola ambapo ameifungia magoli 15 kwenye mechi 18.
Depu ametua Yanga kuchukua nafasi ya Andy Boyeli ambaye mkataba wake wa mkopo ulisitishwa.
Aidha Mshambuliaji huyo ni pendekezo la Goncalves aliyehitaji kuongeza nguvu eneo la safu ya ushambuliaji ambalo msimu huu lilianza kwa kusuasua baada ya Clement Mzize kuumia na hivyo kupelekea Prince Dube kuwa mchezaji pekee tegemeo katika eneo hilo.
