NAFASI 1150 Za Kazi MOWASALAT

NAFASI 1150 Za Kazi MOWASALAT
NAFASI 1150 Za Kazi MOWASALAT
Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano kwa kushirikiana na Kampuni ya Almaha Travel and Tours Company Limited, inawatangazia Watanzania wenye umri kati ya miaka 25 hadi 50 kuwasilisha maombi ya ajira kwa ajili ya kujaza nafasi 1,150 za madereva, zilizotolewa na Kampuni ya MOWASALAT ya nchini Qatar.
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe na Daraja la Leseni C au E.
- Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe na Leseni halali ya Udereva.
- Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) katika fani ya udereva.
- Awe na Hati halali ya Kusafiria (Passport).
- Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiingereza.
- Mwenye uelewa wa lugha ya Kiarabu atapewa kipaumbele.
MASHARTI YA AJIRA
- Ajira ni ya mkataba.
- Mwajiri atalipa mshahara kulingana na sheria za kazi za nchi ya Qatar.
- Gharama za matibabu kwa kipindi chote cha ajira zitagharamiwa na mwajiri.
- Mwajiri atalipia viza na tiketi ya ndege.
- Mwajiri atalipia malazi na chakula kwa kipindi chote cha ajira.
- Mwajiri atagharamia usafiri wa kutoka makazi hadi kituo cha kazi.
- Mwajiri atagharamia viza na tiketi ya kurejea nyumbani baada ya ukomo wa ajira.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Waombaji wote wanatakiwa kutuma Wasifu Binafsi (CV) kupitia barua pepe zifutazo: almaharecruitment696@gmail.com
info@almaha.co.tz
Baada ya kutuma maombi hayo, waombaji wanapaswa kujisajiri kwenye Mfumo wa Kazi kupitia anuani ifuatayo: https://jobs.kazi.go.tz
Mwisho wa Kupokea Maombi ni tarehe 04 Februari, 2026.
