NAFASI 172 Za Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 172 Za Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
NAFASI 172 Za Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya and MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 172 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili hapa chini
✅AFISA AFYA MAZINGIRA MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT ENVIRONMENTALHEALTH OFFICER GRADE II) – Nafasi 172
MAJUKUMU YA KAZI
- Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa.
- Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa ya
kuambukiza. - Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na kuziwasilisha katika mamlaka husika.
- Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili.
- Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii.
- Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha.
- Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo.
- Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira.
- Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi ya Kata na
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo
kinachotambuliwa na Serikali na wawe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.
NGAZI YA MSHAHARA: TGHS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote lazima wawe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.
- Hata hivyo, kwa nafasi za ndani ya Taasisi za Kijeshi: Waombaji wa nafasi zisizo za shahada wasizidi umri wa miaka 25.
- Waombaji wa nafasi za shahada wasizidi umri wa miaka 30.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTVET). Kwa waombaji wa
kada zinazohitaji ‘GPA’ waliosoma nje ya Tanzania waambatishe cheti cha ukokotozi wa ‘GPA’ kutoka TCU. - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
DONWLOAD PDF HAPA
Mwisho wa kutuma Maombi ni tarehe 27 February, 2026.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA, GROUP NO 3 HAPA, GROUP NO 4 HAPA
Tags: NAFASI 172 Za Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II MDAs & LGAs
