NAFASI 1201 Za Madaktari Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI 1201 Za Madaktari Daraja la II MDAs & LGAs
NAFASI 1201 Za Madaktari Daraja la II MDAs & LGAs
✅DAKTARI DARAJA LA II (MEDICAL OFFICER GRADE II) – Nafasi 1201
MAJUKUMU YA KAZI
- Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
- Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
- Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
- Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
- Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
- Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
- Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
- Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
- Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement).
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
NGAZI YA MSHAHARA: TGHS E
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika. - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
