NAFASI Za Kazi Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)

NAFASI Za Kazi Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)
NAFASI Za Kazi Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1979 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008. (“National Construction Council Act, CAP 162, R.E. 2008”).
Baraza hilo lilianzishwa kwa lengo la kusimamia maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini, Katika kutekeleza azma hiyo Baraza linazingatia mahitaji yote yanayokusudiwa kubadilisha sekta kupitia uwekezaji wa teknolojia ya kisasa.
Kwa sasa, Baraza linashughulikia uratibu na uandaaji wa nyaraka zifuatazo:
- Sera ya Sekta ya Ujenzi (CIP);
- Sheria ya Majengo Tanzania;
- Kanuni za Majenzi Tanzania;
- Viwango vya Majengo na Samani za Serikali;
- Uratibu wa Maudhui ya Ndani ya Sekta ya Ujenzi;
- Viwango msawazo vya Majengo na Samani za Serikali.
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Kupitia Ajira Portal, linawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba ajira katika nafasi mbalimbali za kazi zilizoanishwa hapa chini.
- OFFICE MANAGEMENT SECRETARY II (Nafasi 2)
- QUANTITY SURVEYOR II (Nafasi 3)
- INFORMATION COMMUNICATION TECHNOLOGY II – DATABASE ADMINISTRATION (Nafasi 1)
Waombaji wa Ajira hizi wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal.
Kutuma Maombi Fungua tovuti ya Ajira Portal kupitia anwani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/vacancies kisha jaza taarifa zote muhimu kama inavyoelekezwa kwenye tangazo la kazi.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 22/12/2025
