NAFASI 1500 Za Kujitolea Kwa Walimu wa Shule za Sekondari 2026

NAFASI 1500 Za Kujitolea Kwa Walimu wa Shule za Sekondari 2026
NAFASI 1500 Za Kujitolea Kwa Walimu wa Shule za Sekondari 2026
Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM –TAMISEMI) kupitia Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu “Global Partnership for Education Teacher Support Programme(GPE – TSP)” inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea (engagement of volunteer teachers).
Kupitia mradi huu, OWM – TAMISEMI inatangaza nafasi za kujitolea kwa walimu 1,500 wa Shule za Sekondari zilizopo chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa zenye uhitaji mkubwa zaidi kwa kuzingatia utaratibu wa kupanga walimu wa Shule za Sekondari (Secondary Teacher Allocation protocol (S – TAP).
Hivyo OWM – TAMISEMI kupitia mradi wa GPE – TSP inawaalika Watanzania wenye sifa kuwasilisha maombi ya nafasi elfu moja na mia tano (1,500) za Ualimu wa Kujitolea kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.
Nafasi hizi zinalenga walimu wa masomo ya Sayansi na Teknolojia (STEM), Masomo ya Amali (Vocational Subjects) na Masomo ya Biashara
(Business Studies).
Majukumu ya jumla ya kazi ya ualimu wa kujitolea, sifa za waombaji na idadi ya nafasi zimebainishwa hapa chini:-
Majukumu ya Jumla ya Kazi ya Mwalimu wa Kujitolea
- Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na
Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa. - Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia.
- Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi.
- Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani.
- Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi.
- Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu.
- Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule
Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Fizikia (Physics) – Nafasi 504
- Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Fizikia kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu
vinavyotambulika na Serikali au - Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Fizikia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo
vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali au - Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Fizikia kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Kemia (Chemistry) – Nafasi 246
- Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Kemia kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu
vinavyotambulika na Serikali au - Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Kemia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali au
- Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Kemia kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Biolojia (Biology) – Nafasi 332
- Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biolojia kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu
vinavyotambulika na Serikali au - Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biolojia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali au
- Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Biolojia kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
Sifa za Mwalimu wa kujitolea wa somo la Hisabati (Mathematics) – Nafasi 418
- Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali au
- Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Hisabati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo
vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali au - Stashahada ya Ualimu yenye somo la kufundishia la Hisabati kutoka Vyuo vya Ualimu vinavyotambulika na Serikali.
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI
- Awe raia wa Tanzania mwenye namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) na umri usiozidi miaka 43.
- Aambatishe nakala ya cheti cha Kuzaliwa, vyeti vya elimu na Taaluma.
- Awe tayari kufanya kazi katika Shule za Sekondari zenye uhitaji mkubwa wa walimu.
- Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine.
- Awe hajawahi kufukuzwa au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa makosa ya kiutumishi;.
- Waombaji waambatishe nyaraka zote zinazohitajika katika mfumo; na
- Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi
EQ… kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
PDF YA TANGAZO AJIRA ZA MAKATABA GPE TSP
Waombaji wote wenye sifa tajwa hapo juu watembelee tovuti ya OWM – TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz kwenye kiunganishi cha Mfumo wa Ajira TAMISEMI https://ajira.tamisemi.go.tz/ ili kupata kiunganishi kwaajili ya kutuma maombi yao kuanzia tarehe 14 hadi 28 Januari, 2026.
Kwa maelezo ya ziada tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28 Januari, 2026 saa 05:59 usiku.
Tags: NAFASI 1500 Za Kujitolea Kwa Walimu wa Shule za Sekondari 2026
