HESLB Kufunguliwa dirisha la Maombi ya Mikopo ya Stashahada ‘March Intake’ 2025/2026

Filed in Elimu, Makala by on 12.02.2026 0 Comments
Share This Post
HESLB Kufunguliwa dirisha la Maombi ya Mikopo ya Stashahada 'March Intake' 2025/2026

HESLB Kufunguliwa dirisha la Maombi ya Mikopo ya Stashahada ‘March Intake’ 2025/2026

HESLB Kufunguliwa dirisha la Maombi ya Mikopo ya Stashahada ‘March Intake’ 2025/2026

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Dirisha la maombi ya mikopo ya Stashahada kwa ‘March Intake’ mwaka wa masomo 2025/2026

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawatangazia wanafunzi wa stashahada watakaodahiliwa mwezi Machi (March Intake) kwamba dirisha la maombi ya mikopo ya stashahada litafunguliwa kuanzia tarehe 15/02/2026 hadi tarehe 15/03/2026 kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo katika maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa kwenye mwongozo wa stashahada wa mwaka 2025/2026.

Wanafunzi wanaotarajia kujiunga kwenye programu za kipaumbele wanashauriwa kutumia fursa ya kuomba mikopo kwa kuzingatia vigezo vilivyomo kwenye mwongozo unaopatikana www.heslb.go.tz

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *