NAFASI Za Ufadhili wa Masomo nchini Indonesia 2026/2027

NAFASI Za Ufadhili wa Masomo nchini Indonesia 2026/2027
NAFASI Za Ufadhili wa Masomo nchini Indonesia 2026/2027
Wizara imepokea nafasi za ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa Watumishi wa Umma kutoka Shirika la Misaada la Indonesia kwa mwaka wa Masomo 2026-2027 kwenye vyuo mbalimbali nchini humo.
Ili kukamilisha maombi ya “Scholarship” hizo, muombaji awasilishe fomu ya maombi kupitia barua pepe maalum iliyoandaliwa kupokea maombi husika ambayo ni tias.scholarship@nje.go.tz
Kwa taarifa zaidi kuhusu fursa hizo tembelea kiunganishi cha https://tias.kemenkeu.go.id
Wizara inapenda kuwahimiza Watumishi wenye sifa kuchangamkia fursa hizo.
Mwisho wa kufanya maombi ni Machi 30, 2026.
