MAGAZETI ya Leo Jumanne 12 August 2025

MAGAZETI ya Leo Jumanne 12 August 2025
MAGAZETI ya Leo Jumanne 12 August 2025
Klabu ya Yanga na kampuni ya Michezo ya kubashiri ya SportPesa wamesaini mkataba mpya wenye thamani ya Sh21.7 bilioni.
Ilikuwa Julai 27,2022 ambapo pande hizo mbili ziliingia mkataba wa miaka mitatu, uliokuwa na thamani ya Sh12.3 bilioni, uliomalizika mwisho wa msimu uliopita.
Mkataba huo mpya ambao umesainiwa tarehe 11 Agosti 2025 na umekuwa na ongezeko la Sh9.4 bilioni utakaoifanya SportPesa kuendelea kukaa mbele ya jezi za Mabingwa hao.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema kuwa safari ya udhamini wao kwa Yanga ni kutokana na kuamini kwamba ni timu sahihi yenye mashabiki wengi na kwamba itaweza kubadili mpira wa Tanzania.
Naye Rais wa Yanga, Hersi Said ameipongeza SportPesa kwa kuipa nguvu ya kiuchumi timu yao akisema imeisaidia kubadilisha mambo mengi ndani ya klabu hiyo.
