RATIBA ya CHAN 2024, 2024 African Nations Championship

RATIBA ya CHAN 2024, 2024 African Nations Championship
RATIBA ya CHAN 2024, 2024 African Nations Championship
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kwa kushirikiana na Mataifa matatu yatakayoandaa michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 ambayo ni Kenya, Tanzania na Uganda imetangaza Ratiba na viwanja vitakavyoandaa Ufunguzi, mechi ya tatu na nne na ya Mwisho ya Mashindano hayo.
Michuano hiyo itafanyika Kuanzia tarehe 02 hadi 30 Agosti, 2025.
Uwanja wa Benjamin Mkapa wa jijini Dar es Salaam, Tanzania utakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi.
Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda umeteuliwa kuandaa mechi ya tatu na ya nne.
Huku Uwanja wa Kasarani wa Kenya jijini Nairobi utaandaa mechi ya Fainali ya tarehe 30 Agosti 2025.
Zaidi ya hayo, Zanzibar imeteuliwa kuwa mojawapo ya Viwanja vya Waandaji, ni uamuzi ambao unasisitiza dhamira ya CAF ya kupanua wigo na ushirikishwaji wa soka la Afrika.
Miji Wenyeji wa Hatua za Makundi za michuano hiyo ni kama ifuatavyo:
Kundi A | Nairobi, Kenya: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia.
Kundi B | Dar es Salaam, Tanzania: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kundi C | Kampala, Uganda: Uganda, Niger, Guinea, Afrika Kusini, Algeria.
Kundi D | Zanzibar: Senegal, Congo, Sudan, Nigeria.
Kufuatia uamuzi wa Bodi ya Rufaa ya CAF, nafasi ya Equatorial Guinea ilichukuliwa na Kongo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu michuano ya TotalEnergies CAF ya Mataifa ya Afrika, tafadhali tembelea www.cafonline.com
Tags: 2024 African Nations Championship, RATIBA ya CHAN 2024
