MAGAZETI ya Leo Ijumaa 26 September 2025

Filed in Magazetini Leo by on 26.09.2025 0 Comments
Share This Post
MAGAZETI ya Leo Ijumaa 26 September 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 26 September 2025

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 26 September 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Loveness Kisile mwenye Umri wa miaka 30 mkazi wa Mtaa wa Temeke, jijini Mwanza akituhumiwa kutoa taarifa za uongo kwa askari, ndugu, jamaa na marafiki kuwa ametekwa.

Anadaiwa kutoa taarifa kwa mume na ndugu zake kwamba ametekwa na watu watatu waliotaka Sh10 milioni ili wasimdhuru na kuondoa ujauzito aliokuwa nao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, amesema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 24, 2025 saa 5:30 usiku, baada kumpigia simu mume wake, Hosea Lusingwa akidai watu hao walimkamata kwa nguvu, kumfunika uso na kumpeleka kusikojulikana.

‎‎Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi Septemba 25, 2025 Kamanda Mutafungwa amesema kuwa taarifa hizo zilizua taharuki kwa mume na ndugu na kulihangaisha Jeshi la Polisi usiku kucha, kwani awali Loveness alimweleza ‎mume wake kwamba ni mjamzito wa pacha watatu.

‎‎Amesema kuwa mume alitoa taarifa Kituo cha Polisi Nyakato akidai watekaji wanahitaji Sh10 milioni na kama asingefanya hivyo wangemchoma mke wake sindano ya kutoa mimba.

“Baada ya muda mfupi alimjulisha mume wake kuwa mimba imetolewa na watoto wake pacha watatu wamefariki Dunia, akisisitiza atume kiasi hicho cha fedha ili aachiwe huru,” amesema.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *