MAGAZETI ya Leo Jumatano 02 July 2025

Filed in Magazetini Leo, Michezo by on 02.07.2025 0 Comments
Share This Post
MAGAZETI ya Leo Jumatano 02 July 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 02 July 2025

MAGAZETI ya Leo Jumatano 02 July 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Wakati mwaka mpya wa fedha ukianza, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemaliza mwaka wa fedha 2024/2025 kwa mafanikio, ikivuka lengo la makusanyo yake na kuandika historia mpya ya ukusanyaji.

Katika mwaka huo wa fedha, lengo lilikuwa kukusanya Sh31.5 trilioni, ila hadi kufikia Juni 30, makusanyo yalifikia Sh32.2 trilioni, ambayo ni ufanisi wa asilimia 105.

Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuwahi kukusanywa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, ilipowekewa lengo la kukusanya Sh539 bilioni, lakini hata hivyo, ilikusanya Sh531 bilioni, ikiwa ni wastani wa Sh44 bilioni kwa mwezi.

Akizungumza Jumanne, Julai 1, 2025, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema katika mwaka wa fedha ulioshia Juni 30, mamlaka hiyo imeandika historia ya kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi yote 12.

Mwenda, aliyeteuliwa katika nafasi hiyo Julai 2, 2024, ikiwa ni siku moja baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha, amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya TRA na walipakodi.

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *