MAGAZETI ya Leo Alhamisi 10 July 2025

MAGAZETI ya Leo Alhamisi 10 July 2025
MAGAZETI ya Leo Alhamisi 10 July 2025

Watu wawili waliokuwa wakimiliki kiwanda bubu kilichopo Sinza, Dar es Salaam, wamekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kutengeneza biskuti zilizochanganywa na bangi na kuzisambaza katika mikoa mbalimbali nchini.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amethibitisha kukamatwa kwa kiwanda hicho na kuonya kuwa matumizi ya mbinu zisizo za kawaida kama hizo ni tishio kwa afya na usalama wa jamii.
Katika hatua nyingine, DCEA imebaini kurejea kwa mbinu za zamani za usafirishaji wa dawa za kulevya nje ya nchi, hali inayoashiria juhudi za wahalifu kukwepa mkono wa sheria.
Kamishna Lyimo ametoa rai kwa wananchi kuwa waangalifu wanapotumwa au kupokea mizigo kutoka kwa watu wasiowafahamu, na pia kutoa taarifa kuhusu yeyote anayejihusisha na biashara ya dawa hizo, hasa wanaoshirikiana na raia wa kigeni.
Aidha, kati ya Mei na Julai 2025, DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanya operesheni mbalimbali zilizofanikisha kukamatwa kwa jumla ya kilo 37,197.142 za dawa za kulevya.
JE, UNATAFUTA AJIRA LEO?Jiunge na Watanzania Wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini Pamoja na Makampuni Mbalimbali Leo Gusa HAPA
Share Kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki nao wapate Fursa hizi Kila Siku.
