MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs July 2025

Filed in Usaili by on 14.07.2025 1 Comment
Share This Post
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs July 2025

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs July 2025

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs July 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 11-08-2025 hadi 12-08-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili
huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask).
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
    kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
    Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
    Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
    HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
    Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao hawajaona majina yao kwenye tangazo hili wanapaswa kuingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kuona sababu za kutokuitwa kwao ili wasikose fursa wakati mwingine.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
  • Wasailiwa ambao majina yao yanatofautiana katika nyaraka zao wanapaswa kuwasilisha Hati ya
    Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

KUITWA KWENYE USAILI MDAs NA LGAs 14-07-2025

Share This Post

Tags:

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Majina ya walioitwa kwenye usaili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *