KUITWA Kwenye Usaili wa Mahojiano Tume ya Utumishi wa Mahakama August 2025

Filed in Usaili by on 03.08.2025 0 Comments
Share This Post
KUITWA Kwenye Usaili wa Mahojiano Tume ya Utumishi wa Mahakama August 2025

KUITWA Kwenye Usaili wa Mahojiano Tume ya Utumishi wa Mahakama August 2025

KUITWA Kwenye Usaili wa Mahojiano Tume ya Utumishi wa Mahakama August 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kufuatia usaili wa kwanza uliofanyika tarehe 19 Julai hadi tarehe 25 Julai, 2025 katika vituo mbalimbali nchini, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia waombaji wa nafasi mbalimbali walioorodheshwa kwenye tangazo hili kuwa, wahudhurie usaili wa ana kwa ana (Oral Interview) kwa tarehe na vituo vilivyooneshwa kwenye orodha ya majina ya wasailiwa iliyoambatishwa na tangazo hili.

Aidha, kwa wasailiwa wa Kada ya Afisa Mwandishi Mwendesha Ofisi II, Mwandishi Mwendesha Ofisi II na Dereva II wataanza na usaili wa vitendo (practical) na watakofaulu wataendelea na usaili wa ana kwa ana (oral interview) kwa siku hiyo.

Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11 Agosti, 2025 kuanzia saa 2:00 asubuhi na wahusika wote wafike na vyeti halisi vya Elimu, Taaluma, kuzaliwa na kitambulisho chenye picha kinachotambulika na Serikali.

Wasailiwa watakaofika kwenye vituo vya usaili bila kuwa na nyaraka zilizoainishwa ama kufika nje ya muda wa usaili uliopangwa hawatasailiwa.

Aidha, wasailiwa wazingatie kuhudhuria usaili kwenye vituo walivyopangiwa.

Kwa wale ambao hawataona majina yao, watambue kuwa hawakupata nafasi ya kuingia kufanya usaili hatua ya pili.

Kwa Tangazo hili, wote walioomba nafasi za ajira watembelee Tovuti ya Tume (www.jsc.go.tz).

Kwa maulizo zaidi piga simu Na 0734219821 au 0738247341, au tuma
barua pepe: maulizo.ajira@jsc.go.tz

DONWLOAD PDF YA MAJINA HAPA

Share This Post

Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *