NAFASI Za Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji Wapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025

NAFASI Za Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji Wapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025
NAFASI Za Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji Wapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 KWA TANZANIA ZANZIBAR
Kwa madhumuni ya uendeshaji wa uchaguzi mkuu na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, kikisomwa pamoja na kanuni ya 10(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo; –
- Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura.
- Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia kura.
- Makarani Waongozaji Wapiga Kura.
SIFA ZA WAOMBAJI WA NAFASI ZA WASIMAMIZI AU WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe ametimiza umri wa miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu.
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (4) au zaidi na anajua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
- Pia, anayeweza kusoma na kuelewa kitabu cha Maelekezo kwa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura na
- we mkazi wa Shehia au Wilaya anayoomba kufanya kazi.
SIFA ZA WAOMBAJI WA NAFASI YA KARANI MWONGOZAJI WAPIGA KURA
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe ametimiza umri wa miaka 18.
- Asiwe kiongozi wa chama cha siasa.
- Awe mwadilifu, mtiifu na mwenye akili timamu.
- Awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (4) au zaidi na anajua kusoma na kuandika katika lugha ya kiswahili au kiingereza.
- Pia, anayeweza kusoma na kuelewa kitabu cha Maelekezo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura
na - Awe mkazi wa Shehia au Wilaya anayoomba kufanya kazi.
MASHARTI YA JUMLA
- Mwombaji lazima aainishe nafasi anayoomba pamoja na Shehia anayoomba kufanyia kazi.
- Mwombaji awe tayari kufanya kazi katika kituo chochote atakachopangiwa. iii) Mwombaji aambatishe: –
a) nakala ya vyeti vya Elimu ya Sekondari na Taaluma ikiwa anavyo. b) wasifu (CV) ukionesha anuani yake ya makazi, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini wake wawili na namba zao za NIDA au za Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi. - Picha mbili zenye ukubwa sawa na picha iliyomo kwenye pasi ya kusafiria (Passport size) za hivi karibuni.
- Barua ya utambulisho kutoka kwa Shehia katika eneo analoishi.
- Mwombaji ambaye ni mtumishi wa umma apitishe barua yake ya maombi kwa mwajiri wake.
NAMNA YA KUTUMA BARUA YA MAOMBI
BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE ANUANI IFUATAYO:
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Ofisi ya Zanzibar,
Mtaa wa Maisara,
S. L. P. 4670,
ZANZIBAR.
MUHIMU: Maombi yote yawasilishwe katika ofisi za wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya husika kwa Unguja na Pemba. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa hayatafanyiwa
kazi.
BARUA ZOTE ZA MAOMBI ZIANDIKWE NYUMA YA BAHASHA NAFASI ANAYOOMBA MWOMBAJI AKITAJA WILAYA AU JIMBO ANALOTAKA KUFANYIA KAZI NA AAMBATISHE VYETI VYA ELIMU PAMOJA NA MAELEZO YA TAARIFA BINAFSI (CV).
MWOMBAJI ATAKAYEBAINIKA KUWASILISHA TAARIFA ZA KUGHUSHI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 16 AGOSTI, 2025 SAA 9:30 ALASIRI
Tags: NAFASI Za Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi na Makarani Waongozaji Wapiga Kura Uchaguzi Mkuu 2025
